'Mwizi wa Mafuta ya Transfoma' yamemkuta!! apigwa shoti na kupoteza Uhai!


Kijana mmoja anaeshukiwa kuwa muhalifu mwenye umri wa kati alikuwa na siku mbaya usiku wa kuamkia jana (17/05/2017) baada ya zoezi lake la kufanya uhalifu kwenye Miundombinu ya Tanesco kutotimia na kumsababishia kupoteza maisha.

Tukio hili limetokea eneo la Mbagala, Mtaa wa Saku Ilulu na kuthibitishwa na mafundi wa Tanesco na wapita njia waliofurika eneo hilo kuangalia mwili wa kijana huyo ambae hakufamika jina lake mara moja akiwa na majeraha mengi mwilini mwake kuashiria kuunguzwa na shoti wakati wa zoezi lake lililoishia pabaya.

Kumekuwapo na wimbi kubwa la wizi wa vifaa mbali mbali na uharibifu wa miundombinu katika transforma za Tanesco maeneo ya Saku katika siku za hivi karibuni, huku wahalifu wakisemekana kulenga vifaa mbali mbali zikiwemo ‘fuse’ na mafuta ya transforma na hivyo kusababisha matukio mengi ya kukatika umeme na kuchochea matukio ya kihalifu kutokana na maeneo mengi ya Mtaa huo kuwa gizani.

Mkazi mmoja wa Kitongoji cha Saku aliyejitambulisha kwa jina moja la Baba Ibrahim, nae amethibitisha uwepo wa kadhia ya kukatika katika umeme mara kwa mara nyakati za usiku katika maeneo hayo… “ni kweli kabisa ndugu mwandishi,.. matukio ya kukatika umeme mtaani kwetu yamekuwa yakijirudia rudia kila mara katika siku za hivi karibuni,.. hatua ambayo imesababisha matukio mengi ya kihalifu ikiwemo uvamizi na wizi”.. alipasha mpashaji ambae ni mkazi wa miaka mingi wa Kitongoji cha Saku.

Blog yako matukio ilifanikiwa kunasa picha mbili zinazosemekana ni mwili wa mhalifu huyo ukiwa umeharibika vibaya !

ciaooo...!!
...endelea kufuatilia blog www.tanzaniampyamatukio.blogspot.com !

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search