Usalama Mahala pa Kazi: Wafanyakazi Zantel walipotembelea Police Oysterbay katika maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama mahala pa kazi

Meneja wa Afya, Ulinzi na Usalama wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Nashon Mudala (aliyesimama kulia) akifafanua kuhusu alama muhimu za usalama kwa wafanyakazi wa Zantel ambazo wanatakiwa kuzizingatia pindi  wanapokuwa kazini wakati wa ziara fupi katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma. Ziara hiyo ilifanywa na wafanyakazi hao mara baada ya kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya, Mkuu wa Sheria na Manunuzi Zantel, Rehema Khalid (Kushoto) na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.
Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya akizungumza na wafanyakazi wa Zantel walipomtembelea katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kulia ni Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.
Askari wa Usalama barabarani, Wilaya ya Kinondoni S/SGT Rehema (kulia) akieleza kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wafanyakazi wa Zantel katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni ACP Theopista Mallya na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.
Askari wa Usalama barabarani, Wilaya ya Kinondoni S/SGT Rehema (kulia) akieleza kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wafanyakazi wa Zantel katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Waliokaa Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya  ya Kinondoni ACP Theopista Mallya na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur
Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya akizungumza na wafanyakazi wa Zantel walipomtembelea katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani.
Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya akiwaonyesha wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel picha iliyotumwa na wadau wa usalama barabarani inayoonyesha matumizi mabaya ya barabara yanayofanywa na madereva wazembe. Wafanyakazi hao walifanya ziara katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kushoto ni Mkuu wa Sheria na Manunuzi Zantel, Rehema Khalid.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na wafanyakazi wa Zantel mara baada ya wafanyakazi hao kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Hafla hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Kampuni hiyo Msasani jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.  - credit Habari za jamii

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search