Video: Wake 10 wa Marais Barani Afrika.. Mama Magufuli 'Is Second to None" (#Top 10 Most Beautiful Firs-ladies of Africa)
Mama Janet Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni First lady wa aina yake, mwenye sifa za kipekee minongoni mwa wake za marais wengine katika Bara la Afrika.
Ni wazi kwa heshima na umri wake wa ‘umama’ lisingekuwa jambo jema wala haki kumtaja kwenye orodha ya wake za marais ‘wanyange zaidi’ Barani Afrika, ingawa sifa hiyo ameipindukia kwa vigezo vyote... (hata kwa kuangalia picha zake...)
Mama Magufuli akiwa na Rais wakisalimiana na Mama Salma na pembeni ni Mama Sity Mwinyi |
Mama Janet ni mama 'asiyejua kununa' (ever smiling, and charm), pengine kwa asili ya kazi yake ya wito ya Ualimu. Ni mwenye uvumilivu wa hali ya juu na aliyejitoa kuzijua shida za Watanzania wote kwa matendo yake mema. Ni msikivu na mvumilivu (down to earth & humble).
Ni Mke wa Rais asiye na majivuno na anayeishi maisha ya Watanzania wa kawaida, akishiriki huduma za kijamii zinazotumiwa na Watanzania wengi ikiwemo Hospitali ya Muhimbili aliyokwenda kutibiwa na kulazwa kinyume cha matarajio ya wengi.
Mama Magufuli ni Mke wa Rais pekee miongoni mwa wake wengine wa Marais Barani humu ambae kwa kujituma kwake kumepelekea miito kutoka kwa wanaharakati mbali mbali kupaza sauti kuwashawishi Wabunge waandike rasimu ya kurasimisha na kuidhinisha ofisi ya uwepo wa ofisi ya Mke wa Rais kama ofisi rasmi ya Umma (The Government of Tanzania, First Lady‘s Office)
Kwa sifa na vigezo hivi ukilinganisha na wake wengine za marais Barani humu, wazungu husema; ‘she is second to none’ kwa maana kwamba hata kama ni wa pili, lakini hakuna wa kwanza nyuma yake! ndio kusema.... she is no.1
No comments:
Post a Comment