Coolest Stuff: Kisa cha Flamingo kusimamia mguu mmoja ?

Flamingo hutumia nguvu kidogo wanaposimama kwa mguu moja, wanasayansi wamethibitisha.


Huenda ndivyo walivyozoeleka kuonekana wakisimama hivyo, lakini vipi na kwanini ndege hao husimama kwa guu moja bado ni kitendawili cha muda mrefu.
Sasa kundi kutoka Marekani limeonyesha kuwa flamingo hawatumii misuli yoyote wanaposimama kwa guu moja jambo linalomaanisha kuwa hawatumii nguvu.
Ni hali inayowaruhusu kusimama hivyo kwa madha ahuku wakisinzia.
Awali watafiti walishangaa iwapo kusimama hivyo kunasaidia kupunguza uchofu wa misuli wakati ndege hao walibadili kutoka kusimama kwa guu moja hadi jingine.
Makundi ya watafiti wengine yamegundua kuwa hali hii huwasaidia ndege hao kusawazisha ujoto wa mwilini.
Sasa profesa Young-Hui Chang, kutoka taasisi ya teknolojia ya Georgia (Georgia Tech) huko Atlanta, na Lena H Ting, wa chuo kikuu cha Emory, wamegundua siri ya mbinu hiyo.
Watafiti hao waliwafanyia uchunguzi kadhaa ndege walio hai na waliofariki. Na wamegundua kuwa Flamingo wanaweza kusimamishwa kwa gu moja pasi usaidizi wowote.
"Unapomtizama ndege huyo usoni, anaposimama kwa guu moja, mguu uko chini ya mwili inayomaanisha kuwa mguu umejipinda kwa ndani. Inabidi usimame hivyo iliwa kuweza kuidhinisha mfumo wa kutua," Prof Chang ameiambia BBC.
Hatahivyo, ndege waliokufa hawawezi kusimama kwa miguu miwili, inayomaanisha jukumu kubwa la kutumika misuli katika kiwango hichi.
Watafiti hao pia waliwachunguza ndege walio hai, na kugundua kwamba wanaposimama kwa guu moja na kupumzika hawakusogea hata chembe. Jambo linalothibitisha u thabiti wa kusimama kwa aina hiyo - bbcswahili.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search