10 News!!: Diamond Platnumz 'apeleka jibu' BASATA 'afunga kazi Airport' akimpokea Ray Vanny.. #share.. Tanzania yachukizwa na Kenya kuzuia Gesi ya Kupikia.. RITA nayo 'Yaliamsha' yataka Maalim Seif athibitishe..

Mwanamuziki wa Tanzania alieng'ara kwenye tuzo za BET Awards zilizofanyika Nchini Marekani hivi karibuni, amewasili Jijini dar es Salaam jana na akipokelewa na Diamond alieongozana na Maelfu ya Mashabiki wake. 



Mapokezi ya Diamond yalionekana kama jibu kwa BASATA ambayo awali iliweka bayana kuwa haina mipango yoyote ya mapokezi rasmi kwa Ray, ambae licha ya mafanikio yake kwenye kipengele 'Mwananamuziki Bora Chipukizi wa 2017 katika Anga za Kimataifa, hakuwa ameitaarifu BASATA wakati wa safari yake hiyo ya matumaini, wala safari yake ya kurudi baada ya kupokea Tuzo yake hiyo ya kwanza kabisa kuchukuliwa na mwanamuziki wa Tanzania, na ya pili Africa Mashariki baada ya ile ya Eddy Kenzo wa Kenya Mwaka 2015. 

Diamond alieongozana na Harmonize, na kundi zima la Wasafi na maelfu ya washabiki waliwasili uwanjani hapo na kufanya shughuli kusimama kwa furaha na bashasha huku kila aina cheers zikisikika..










About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search