Dk. Kigwa aja na mapya ya ‘makinikinia..' #share.. asema waliposema ‘walikimbizwa kama wezi..’
Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye pia
ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ameweka
wazi kuwa daima ataendelea kupambana dhidi ya rasilimali za umma, kwani amekuwa
mwanaharakati kwa muda mrefu.
“Tuliopinga wizi wa madini yetu tulibezwa, tulikamatwa kama
wezi; tuliswekwa ndani, tulionekana wasaliti. Leo kiko wapi?
#NasimamaNaRaisWangu” aliandika Dk. Kigwangalla huku watu mbalimbali wakitoa
maoni yao.
Kwa mujibu wa Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, suala la
kupambana na rasilimali za Taifa alilianza miaka mingi kwani miongoni mwa
matukio makubwa ni la 2013, ambapo alijitolea kupambana kudai haki tukio
lililopelekea kutiwa nguvuni na Jeshi la Polisi.
Dk. Kigwangalla anasema katika kupigania maslai Taifa
ataendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Magufuli mwanzo mwisho kwani ni moja
ya matunda ya nchi yoyote ile Duniani.
Anasema kiongozi Mkuu lazima alinde na kupigania rasilimali
za nchi, hivyo akiwa Mtanzania na kiongozi mwenye dhamana anaunga juhudi hizo
bila kuchoka – CR. JJMSACKY
No comments:
Post a Comment