JPM apiga 'dongo' kiaina.. #share.. Azindua Mtambo wa Maji Ruvu Juu..
"Ukishajenga viwanda, barabara zitakuja tu, Ukishaoa mwanamke ukamuweka ndani lazima mtoto atapatikana tu labda na wewe uwe mkwere" - JPM pic.twitter.com/tXlRed19Aw— AzamTV (@azamtvtz) June 21, 2017
Rais John Magufuli leo ameendelea na ziara yake Mkoani Pwani na amefungua kuzindua mtambo wa maji wa Ruvu Juu ambao unasambaza maji katikana mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.
Mtambo huo ambao ni wa pili kwa ukubwa baada ya Ruvu Chini umepanuliwa na kuuwezesha kuzalisha maji kiasi cha mita za ujazo 196,000 kutoka kiwango cha mita za ujazo 82,000 ilizokuwa inazalisha zamani.
Maeneo yanayonufaika na mradi huo ni yale yaliyo kandokando ya bomba ambayo ni Mlandizi, Visiga, Kongowe, Kiluvya, Kibamba, Mbezi na Kimara.
Maeneo mengine ni Changanyikeni, Ubungo, Kibangu, Makuburi, Tabata na Segerea.
No comments:
Post a Comment