Maalim Seif alivyofanikisha Harambee ya Madrasat-L-Muuminin Kiwalani.. #share.. mamilioni yakusanywa..


Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akikabidhi mchango wake wa shilingi laki tatu katika harambee ya kuchangia Madrassa ya Muumini Islamiya iIliyopo kiwalani Dar es Salaam


Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akikabidhi mchango wake kwa Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwa ajili ya Muumini islamiya.

Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiongoza harambee ya uchangiaji wa Madrasa Kiwalani Temeke jijini Dar es Salaam ambapo aliwezesha kupatika kwafedha zaidi ya Milioni 7 kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja kipya cha Madrasa hiyo


Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza wakati alipokuwakitoa ahadi yake ya Milioni moja kwa ajili ya Madrasa hiyo na aliweza kuwasilisha shilingi laki tano papo hapo na kuongeza ahadi ya bati 70 na mifuko 50 ya Saruji.


Diwani wa Kata Mianzini , Kassim Mshamu ambaye ndio mlezi wa Madrasa ya Muunin Islamiya akiwakaribisha wageni katika arambee yakuchangia madrasa


Sheikh Anuary Jongo akitoa Darasa juu ya waslamu na umuhimu wa kuchangia nyumba za ibada hili waweze kujenga ukaribu na Mungu hasa katika kumi hili la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani


Sehemu ya washiriki wa arambee hiyo wakipata futari iliyoandaliwa na Madrasa Muumin Islamiya


Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiteta na Mkurugenzi wa uchaguzi wa Chama Cha Wananchi CUF , Shaweji Mketo


Sehemu ya watoto wa Madrasa ya Muumini Islamiya wakipata futari mara baada ya kumalizika kwa harambee hiyo


Vijana wa Kiislamu wakitoa Nashid kwa ajili ya kuleta burudani kwa watu waliofika katika arambee hiyo


sehemu ya vijana wa Madrassa ya Muumin Islamiya wakinyosha mikono wakati wa utambulisho


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search