Ziara ya JPM ilivyogeuka 'Limao' kwa Mutalemwa wa DAWASA #share..

Katika ziara ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoendelea katika Mkoa wa Pwani, jana alipata fursa ya kuzindua rasmi mtambo wa kusafisha na kusukuma maji wa Ruvu Juu, Mlandizi mkoani Pwani, shughuli ambayo pia imehudhuriwa na wawakilishi wa Benki ya Dunia, nchi za India na China. 

 Akiongea katika uzinduzi huo, Rais Magufuli, alieonekana wazi kukerwa na kasi ndogo ya mambo yanavyokwenda ndani ya Dawasa, alimtaka Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ya Maji Safi na maji taka Dar es Salaam, Archad Mutalemwa kustaafu kwa hiyari yake kwa sababu ameitumikia nchi kwa muda mrefu. 

Akaongeza kwamba asisubiri aondolewe kwa kashfa kwa sababu ukifanya kazi kwa muda mrefu, kuna uwezekano mkubwa wa kukwaa kashfa mbalimbali, akasisitiza kwamba faili la Mutalemwa analo mezani kwake na kwamba anamfahamu vizuri.

Kama ulipitwa na hotuba ya Mhe. Rais kwenye uzinduzi huo.. fuatana na maktba ya matukio kupata yaliyojiri..
 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search