Mazishi ya 'Mbunifu Nembo ya Taifa,.. Wanafamilia waishukuru Serikali kuwakutanisha!!!



Leo Jumapili ya tarehe 04/06/2017 itabakia kuwa siku ya kukumbukwa katika kumbukumbu muhimu ambapo 
mzee Francis Kinyasu anayeaminika kuwa mbunifu wa nembo ya Taifa amehifadhiwa katika 'nyumba yake Milele..! katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Nange, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza na kuhudhuriwa na mkusanyiko mkumbwa wa ndugu, jamaa, na Viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela.

Akizungumza wakati wa mazishi hayo mbele ya Bwana Mongella, dada wa marehemu, Mwakami Nhinyale ameishukuru serikali kwa kufanikisha kuurejesha mwili wa ndugu yake aliyesema wamepotezana tangu mwaka 1976.

 Kwa mujibu wa dada huyo, licha ya kutorejea nyumbani tangu miaka hiyo ya sabini, marehemu pia hakuwa na mawasiliano na ndugu zake hadi walipopata taarifa zake za kuugua na kufariki kupitia vyombo vya habari. Alisema katika tumbo la mama yao, Ng'hayiwa Buyabila walizaliwa watoto wanne kwa baba mmoja, Nhinyale Buyabila. 

"Licha kuzaliwa na mama mmoja, marehemu alizaliwa kwa baba mwingine ndiyo maana ana ubini tofauti"‎
Mcl online

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search