'Zoa zoa ya Mnyika Bungeni yazua mapya... LHRC wataka Katiba ya Wananchi..

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Ubungo kimesema hatua ya Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika kutolewa kwa nguvu Bungeni Juni 2, si kitendo cha Kiungwana. Katibu Mwenezi wa Chadema Ubungo, Perfect Mwasiwelwa amesema Wapinzani akiwemo na Mnyika wamekuwa watetezi wa masuala ya madini kwa miaka takribani 20 ila sasa wanaonekana sio wazalendo wa Taifa lao.


"Kitendo cha Mnyika kubebwa mzobemzobe na kutupwa nje ya mlango wa bunge na ukiangalia mazingira alitaka kudondoka, kwakweli ni kitendo cha kinyama, sio cha kiungwana, sio cha kibinadamu na Kitanzania kabisa," amesema Mwasiwelwa.
Amesema kuwa Chadema inapinga nguvu inayotumika kuzima upinzani kupigania suala la madini kama ilivyofanyika kwa Mnyika ambaye ni Waziri kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini.

Wakati huo huo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeishauri serikali kuendeleza mchakato wa kupatikana kwa katiba ya wananchi ambayo italeta mabadiliko ya sheria katika sekta ya maliasili, madini na ardhi ili kila mtanzania aweze kunufaika na rasilimali za nchi

Tamko hilo limetolewa jana na Afisa Program wa kituo, Pansias Mloe kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, wakati wa ziara ya wafanyakazi kwenye mbuga ya hifadhi ya Saadan ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.

Alisema kuna vivutio vingi vya utalii havijarasimishwa vyenye uwezo wa kuongeza mapato kwenye sekta hiyo, hivyo Ni mda muafaka kwa serikali kufanya kazi eneo hilo...

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search