News: TLS wapinga kuundwa kwa Bodi ya Usajili wa wanasheria,.. #share wasema itawanyima weledi..

CHAMA cha Wanashreria wa Tanganyika (TLS) kimepinga pendekezo la kuundwa kwa Bodi ya Usajili wa wanasheria nchini itakayokuwa chini ya Waziri Wa Katiba na Sheria kwani ina lengo la kuwanyima Uhuru mawakili katika kutekeleza majukumu yao kwa mujibu Wa taaluma.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais wa Chama hicho Tundu Lissu wakati wa ufunguzi  wa mkutano wa wanachama wa TLS na viongozi wao wenye lengo la kujadili na kuja na njia ya jinsi ya kukabiliana na suala hill kwani likitimia watakuwa wanaingiliwa.

Aidha Lissu alisema kuwa bodi hiyo ikiundwa Waziri ndiye atakayekuwa na mamlaka ya kuwawajibisha mawakili katika masuala ya kinidhamu hali ambayo itakuwa vigumu kwao kutetea mahakamani watu ambao watakuwa wanaikosea serikali. 

“Kitu kinachopendekezwa, hiki kinachoitwa 'Bango Kitita' lengo lake ni kuuwa chama cha mawakili lakini vile vile kufanya masuala yote yanayohusu utetezi wa watu mahakamani; namna mawakili watakavyofanya kazi wadhibitiwe na Serikali kupitiwa Waziri Wa Katiba na Sheria," alisema Lissu.

Lissu alisema kuwa katika kipibdi chote ambayo kumekuwa na mawakili, mamlaka yao yamekuwa yakidhibitiwa napande kuu Tatu ambazo ni Mahakama, Jaji Mkuu na Msajili wa mahakama kuu na upande Wa Serikali kupitia ofisi ya mwanasheria mkuu Wa serikali pamoja na TLS.

Alibainusha kuwa  kuundwa kwa chombo hicho hicho siyo tu kunaipa mamlaka ya serikali kuwadhibiti mawakili bali pia kunampa mamlaka ya moja kwa moja na waziri, hivyo alisisitiza kuwa chombo hicho kikiundwa watakuwa wamekwisha pamoja na wananchi wanaohitaji huduma yao.

Kutokana na hali hiyo alibainisha kuwa amewausia wanachama  wahakikishe kwamba wanalinda uhuru wa Chama cha mawakili wa Tanzania na walinde maisha kwa sababu wanachokabilana nacho kwa sasa ni tishio la kifo kwa taluuma ya sheria nchini.

Aidha alisema nambo ambayo aliwaomba wanachama ni kupigania kwa nguvu zao zote katika kuhakikisha  uwepo wa TLS pamoja na kupigania uhuru wa taaluma ya sheria.

Alisama Tanzania imesaini mikatab mbali mbali ya kimataifa na azimio la baraza la Umoja wa Mataifa ambayo inataka taaluma ya sheria iwe huru pasipo kuingiliwa na watawala wala wanasiasa.

Alieleza kuwa maazimio hayo yanataka nchi wanachama kuhakikisha wanasheria wanakuwa na haki ya kuunda na kijiunga na vyama vyao vya kitaaluma ambavyo vitaruhusiwa kuendesha mambo yao bila kuingiliwa.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search