AY na Mwana-FA wazidi kuigaragaza Tigo Mahakamani,.. sasa 2.1 Billion njia nyeupee !! #share

Harakati za kampuni ya Mic Tanzania Limited kujinasua na utekelezaji wa hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala inayowataka kuwalipa fidia ya Sh2.1 bilioni wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwinyijuma (MwanaFA) na Ambwene Yesaya (AY) zinazidi kugonga mwamba.



Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imelikataa ombi la kampuni hiyo kukata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo iliyolitupa ombi lake la kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo.

Mahakama ya Wilaya ya Ilala katika hukumu ya mwaka jana iliiamuru kampuni hiyo iwalipe fidia ya kiasi hicho cha fedha wasanii hao kwa makosa ya ukiukwaji wa hakimiliki.
ya simu bila makubaliano wala ridhaa yao. Nyimbo hizo ni Usije mjini wa MwanaFA na Dakika moja wa AY.

Kampuni hiyo ilikata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu hiyo na pia iliwasilisha maombi ikiomba kusimamishwa utekelezaji wa hukumu hiyo hadi uamuzi wa rufaa utakapotolewa.

Wasanii hao kupitia wakili Albert Msando waliweka pingamizi wakiiomba Mahakama Kuu itupilie mbali maombi hayo, wakidai ni batili kwa kuwa yamefunguliwa chini ya kifungu cha sheria kisicho sahihi.

Ijumaa, Mahakama Kuu katika uamuzi uliotolewa na Jaji Isaya Arufani iliyatupa maombi ya kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo baada ya kukubaliana na hoja za pingamizi za Msando 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search