Sakata la Mwandishi Elias Mhegera kumpiga risasi Baba Mkwe wake laibua mapya.. Polisi wasema ni 'ishu ya kifamilia..' #share

Imeelezwa kwamba chanzo cha mwandishi wa habari wa kujitegemea, Elias Mhegera kumpiga risasi baba mkwe wake kanisasni juzi ni hisia kuwa mzazi wa mwanamke huyo ndiye chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yao miaka 10 iliyopita. 

Mhegera ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu juzi amekuwa katika mvutano wa muda mrefu na mke wake ambaye waliachana miaka 10 iliyopita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majuzi majira ya saa1:30 asubuhi katika Parokia ya Bikira Maria, Kibangu na kueleza kuwa chanzo ni ugomvi wa kifamilia.

“Adrian Mpande alijeruhiwa bega la kushoto na mtu anayedaiwa kuwa ni mkwe wake. Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa sababu ni mambo ya kifamilia,” alisema Kamanda Kaganda na kuongeza: “Tunaendelea na uchunguzi na kukiwa na umuhimu tutawaeleza kwa uwazi.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa Mzee Mpande alipigwa risasi mbili wakati akijiandaa kuingia kanisani kwa ibada juzi Jumapili.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search