Balozi Mahiga aweka msimamo Kuhusu Tanzania kuingilia Uchaguzi Mkuu Nchini Kenya.. #share
Waziri wa Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustino Mahiga amekanusha taarifa zinazoishutumu Tanazania kuwa na mipango ya kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge wa Kenye unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo.
Siku za Hivi karibuni kumekuwapo na tarifa kwenye vyombo vya habari vya Kenya na Tanzania pamoja na Mitandao ya kijamii ambazo zimekuwa zikieneza uvumi kuwa Tanzania itaingilia uchaguzi wa Kenya.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Waziri Mahiga amewahakikishia serikali ya Kenya, wananchi wa Kenya na Watanania kuwa serikali ya Tanzania haitaingilia uchaguzi huo.
"Napenda kusema kwa niaba ya serikali yetu kuwa tanzania ni nchi ambayo inapenda amani kutoka kwa mataifa rafiki hivyo haiwezi kuingilia uchaguzi kutoka katika nchi nyingine na uvumi huo ni michezo michafu ya baadhi ya watu katika kuchochea machafuko ya kisiasa ,"alisema Mahiga.
Aidha amewataka watanzania kutokubaliana na tuhuma hizo zinazofanywa na baadhi ya vyama pinzani baini ya nchi ya Kenya na Tanzania katika kutoa na kueneza taarifa zisizo sahihi ili kuweka chuki miongoni mwa nchi hizo.
Alibainisha kuwa vyuombo vya dola vinafuatilia suala hilo na watakaobainika kueneza uvumi huo watachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande mwingine Waziri Mahiga amesema kuwa Tanzania na Kenya zimekubaliana kwa pamoja kuondoa vikwanzo vya kibiashara vilivyokuwepo hapo awali na kwamba kumeundwa tume maalumu ya kukabiliana kuondoa vikwanzo vya kibiashara vitakavyojitokeza na kufanyia ufumbuzi ili kukabiliana na changamoto hizo.
Amesema tume hiyo itaongozwa na mawaziri wa mambo ya nje na mawaziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki wa Biashara,Fedha,Mambo ya Ndani,Uchukuzi,Kilimo na Utalii.
"Mawaziri wataunda mfumo wa kuchukua taarifa na kuzitatua ili zisiweze kujirudia kwa lengo la kukuza ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizi zote mbili katika kuwa na umoja wa kibiashara na kuepuka tofauti hizo, nawaomba wafanyabiashara kuwa wavumilivu," alisema Mahiga.
No comments:
Post a Comment