Biashara: Pitia Taarifa ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa wiki iliyoishia Julai 21 mwaka huu.. #share

Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)

Thamani ya mauzo ya hisa kwa wiki hii yamepanda kwa 7% kutoka Shilingi bilioni 3.9 wiki iliyopita hadi Shilingi bilioni 4.1 wiki hii iliyoishia tarehe 21 Julai 2017.

Japokuwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeshuka kwa 29% kutoka hisa milioni 17 wiki iliyoisha tarehe 14 Juni 2017, hadi hisa milioni 12 kwa wiki iliyoishia 21 Julai 2017.

Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:

CRDB …………………………………………..……57%

TBL ……..…….………………..…………..………33%

SWISSPORT …….....……….……....………… 3%

Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)

Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umeshuka kwa Shilingi Bilioni 666 kutoka Shilingi Trilioni 19.2 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 18.5 wiki iliyoishia tarehe 21 Julai 2017. Hii ni kutokana na kushuka kwa bei za hisa za KA (28%), ACA (16%) na TCCL (15%).

Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umeshuka kwa Shilingi Bilioni 18 kutoka Shilingi Trilioni 7.72 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.70 wiki hii. Hii ni kutokana na kushuka kwa bei ya hisa za TCCL (15%), DCB (1%) and TPCC (1%).

Hati Fungani (Bonds)

Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 21 Julai 2017 yamepungua kutoka Shilingi bilioni 44.3 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 35.2

Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na mbili (12) za serikali na za Makampuni binafsi (Corporate Bonds) zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 40.5 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 35.2.


Viashiria (Indices)

Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepungua kwa pointi 76 kutoka pointi 2,211 hadi pointi 2,134 kutokana na kushuka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni.

Kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepungua kwa pointi 8 kutoka pointi 3,673 wiki iliyopita hadi pointi 3,664 wiki hii.

Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) kimepungua kwa pointi 16 kutoka pointi 4,809 hadi pointi 4793, hii imechangiwa na kushuka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilipo sokoni.

huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii kimepungua kwa pointi 0.4 kutoka pointi 2,616 hadi pointi 2,615 kutokana na kushuka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilipo sokoni

Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imepanda kwa pointi 8 kutoka pointi 2,467 Hdi pointi 2,475 baada ya hisa za Swissport kupanda kwa 0.5% kutoka shilingi 3,800 hadi 3,820 kwa hisa moja.

Shindano la Wanafunzi la Uwekezaji

Shindano la DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2017 lilifika mwisho tarehe 30 Juni 2017. Zaidi ya wanafunzi wa vyuo na secondary 12,000 walishiriki katika shindano la mwaka huu, ikiwa ni Zaidi ya mara 3 ya mwaka uliopita, 2016.

Matokea ya washindi wa shindano hili yalitangazwa tarehe 18 July 2017 baada ya kufanyika tukio la mwisho la kuhusisha wanafunzi 10 bora kushiriki katika kipindi cha maswali na majibu na washindi watatu (3) kuamuliwa na jopo ya majaji wa shindano hili.

Wafuatao ndio walio ibuka washindi wa shindano kwa Shule za Sekondari na Vyuo Vikuu.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search