Biashara: Dk. Mpango azitaka Taasisis za fedha kulipa kodi, kuepuka mkono wa serikali kuchukua hatua za kisheria dhidi yao..#share.
WAZIRI
wa Fedha na Mipango Dk. Phillip Mpango amezitaka Taasisi zote zinazotoa huduma
za kifedha nchini kuhakikisha zinalipa kodi stahiki ili kuepuka mkono wa
serikali kuchukua hatua za kisheria dhidi yao.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salam wakati ufunguzi wa Kongamano la tatu la
huduma za kifedha vijijini ulioandaliwa na Taasisi za Huduma za Kifedha nchini
(TAMFI), Mpango alisema taasisi hizo zimekuwa zikitoa mikopo kwa riba kubwa
huku hazilipi kodi.
“Kodi hizi ni kwa ajili ya maendeleo ya Taifa, hivyo niwatake
wahusika wote wachukue hatua kujirekebisha kabla ya mkono wa sheria
haujawafikia,” amesema Dk. Mpango.
Aidha
katika mkutano huo ambao unalenga kujadili namna ya kumsaidia mkulima kuweka
vivutio vya kiuchumi hususani kwenye mazao ya shambani, Mpango alizitaka
taasisi hizo za fedha kuhusisha pia wadau mbali mbali wanaoweza kuongeza
thamani za mazao ya kilimo.
Mpango
ameziomba kutoa mikopo yenye mashariti nafuu kwa wajasiria mali wadogo na
wakati pamoja na kuwapatia elimu ya namna ya kukopa na kuitumia kwa maendeleo
ya kiuchumi badala ya kuitumia kwenye anasa pamoja na jinsi ya kuirudisha kwa
wakati.
Aidha ametoa rai kuwa kwa vikundi vyote vyenye rekodi nzuri ya
kurejesha mikopo kwa wakati waona umuhimu wa kuwakopesha kwa masharti nafuu
ambapo alitoa mfano kwa vikundi vya wanawake ambavyo vina rekodi ya 98% ya
kurejesha mikopo kwa wakati.
Amezitaka
pia kuwa na tabia ya kufuatilia maendeleo ya miradi ambayo wanaitolea mikopo
pasipo kusubiri ife kwani hiyo itawasaidia kujua changamoto mbali mbali zinazowakabili
wakapeshwaji nakuweza kuwasaidia.
Pia
ameshauri kuwepo na utaratibu wa kutoa mikopo kwa njia ya teknolojia ya habari
mfano kwa njia ya mtandao ambayo inarahisisha katika utoaji wa mkopo kwa mda
mfupi hata kwa mtu aliyembali.
Amewahakikishia
kuwa serikali itahakikisha panakuwepo na sera nzuri na taratibu za utoaji wa
huduma ndogo ndogo za kifedha ambapo alisema sera hiyo itakuwa imekamilika
kabla ya mwezi Juni mwakani.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment