Big News: Hatimaye Halima Mdee aachiwa kwa dhamana mchana huu.. ni baada ya kusota rumande kwa zaidi ya masaa 144 #share Mzee Mkapa 'azidi' kuwachanganya 'wapumbavu'.. Papa Francis 'atishwa' na 'muungano mpya' wa Marekani na Russia...

 Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 na wadhamini wawili. Ushahidi haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi August 7, 2017.



Hapo awali, Mbunge huyo kijana wa kambi ya upinzani aliswekwa rumande kwa amri ya Mhe. DC wa Kinondoni Bw. Ally Happi aliemshutumu Mhe. Mdee kwa kosa la kutoa lugha ya 'dharau' kwa Mkuu wa Nchi, ambapo alitumia sheria inayompa mamlaka ya kumuweka ndani mtuhumiwa kwa muda usiozidi masaa 48.
Hata hivyo, pendine kutokana na kuingiliana na mapumziko ya mwishoni mwa wiki, inasemekana Mhe. Halima amesota ndani kwa muda wa masaa zaidi ya 144.
Akielezea mazingira Kaimu Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lucas Mkondya alinukuliwa akisema: "Mhe. Halima mdee tulimkamata maeneo ya Ubungo kwa sababu alikua na kikao na waandishi wa habari akipinga maamuzi ya Rais". 

==== ===========

Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa amefunguka na kusema tafiti zilizotolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Ally Mwalimu zitawafungua kidogo wale watu aliowaita wapumbavu kipindi cha kampeni za



Mhe. Mkapa amesema hayo leo alipokuwa wilayani Chato mkoani Geita wakati akikabidhi nyumba 50 zilizojengwa na taasisi yake The Benjamin William Mkapa Foundation (BMF)na kusema kwa takwimu mbalimbali zilizotolewa na waziri kwa upande wa sekta ya afya tu kunatosha kuwapunguza upumbavu watu aliowahi kuwaita wapumbavu ambao ni wapinzani.
"Kwa takwimu alizotoa Waziri wa Afya juu maendeleo ya afya nchini na mipango ya afya tu, naamini itapunguza kidogo 'Upumbavu' wa wale niliowahi kuwaita wapumbavu siku za nyuma" alisema Mkapa

Mbali na hilo Rais mtaafu alieleza sababu kadhaa zilizomfanya kumteua kwa mara ya kwanza John Pombe Magufuli kuwa Naibu Waziri na baadaye kumteua kuwa Waziri kabisaa kuwa ni pamoja na uchapaji kazi wake

"Mimi nilimteua Magufuli kuwa Naibu Waziri na baadaye kuwa waziri kutokana na utandaji wake wa kazi, nguvu zake na hali yake ya kufanya kazi, kwani alikuwa ni mtu mwenye upendo wa dhati na kujali kile anachokifanya" alisema Rais Mstaafu Benjamin Mkapa
Aidha Mkapa alisema yeye ni Rais mstaafu lakini hajastaafu kukitumikia chama chake Chama Cha Mapinduzi na kusema hawezi kuja kuondoka ndani ya CCM mpaka siku malaika wa mbinguni watakapokuja kumchukua.

"Mimi sijastaafu mapenzi ndani ya Chama changu cha CCM, nitaendelea kukitumikia chama changu mpaka siku Mungu atakaponiita, ndiyo nitaacha kukutumikia chama" alisema Benjamin Mkapa

Rais Mstaafum Benjamin Mkapa mwaka 2015 katika uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi aliwasema kuwa watu wanaojiita ni chama cha ukombozi ni wapumbavu kwani Tanzania tayari ilishakombolewa na ASP na TANU - EATV













About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search