NEWS: Baada ya 'kuanguka' Wakati wa Sikukuu ya Eid-l-fitr Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE) Leo wametuletea hii... #share..
THAMINI ya mauzo ya hisa katika Soka la Hisa la Dar es Salaam (DSE) katika wiki iliyoishia Julai 6 mwaka huu imeongezeka kwa mara 15 zaidi ya ilivyokuwa wiki iliyopita kutokana na kushuka kwa asilimia 98.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mwandamizi wa DSE Mary Kinabo akizungumza na waandishi wa habari, amesema mauzo hayo yameongezeka kutoka Sh. milioni 412 wiki iliyopita hadi Shilingi bilioni 6.
“Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imepanda kutoka hisa 335,000 wiki iliyoisha Juni 30, 2017, hadi hisa milioni 13.6 kwa wiki iliyoishia Julai 6 mwaka huu,” amesema Kinabo.
Alibainisha mauzo hayo kuwa ni Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) asilimia 53.8, Benki ya CRDB asilimia 43.8 na Benki ya NMB asilimia 0.84
Aidha alieleza kuwa ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umepungua kwa Sh. bilioni 566 kutoka Sh. trilioni 19.2 wiki iliyopita hadi Sh. trilioni 18.7 wiki iliyoishia Julai 6 ambapo alibainisha kuwa hali hiyo inatokana na kushuka kwa hisa za Kampuni ya USL (13.33%), KA (6.6%) na ACA (5.9).
Alisema kwamba ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepungua kwa Sh. bilioni 52 kutoka Sh. trilioni 7.75 wiki iliyopita hadi Sh. trilioni 7.70 wiki hii na hiyo ni kutokana na kushuka kwa bei ya hisa za TBL (2.99%).
Akizungumzia kuhusu hati fungani alieleza kuwa kama ilivyokuwa kwa hisa, mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia Julai 6 pia yamepanda kutoka Sh. bilioni 9.6 wiki iliyopita hadi Sh. bilioni 12.25
Kilabo alifafanua kwa kusema mauzo hayo yalitokana na hatifungani kumi na sita (16) za serikali na za Makampuni binafsi ( Corporate Bonds) zenye jumla ya thamani ya Sh. bilioni 13.39 kwa jumla ya gharama ya Sh. bilioni 12.25.
Kwa upande wa Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepungua kwa pointi 65 kutoka pointi 2,217 hadi pointi 2,151 kutokana na kuongezeka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni.
No comments:
Post a Comment