Big news !! Madam Wema atua Kisutu na mama'ke pembeni.. Rais Mstaafu Mkapa akabidhi nyumba za Mkapa Foundation.. #share.. Salamu za mwisho za Lukaku kwa mashabiki wake wa Everton..

Msanii wa Filamu za bongo Wema Sepetu asubuhi ya leo aliwasili mbele ya Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, pembeni yake akiwa ni mama yake mzazi.. 'mama wema...' 
Hata hivyo shauri lake limepigwa kalenda na amepangiwa kufika tena Mahakamani hapo siku ya tarehe 1/August. 
Madam Wema alifika Mahakamani hapo kusikiliza kusikiliza kesi ya kukutwa na dawa za kulevya, kesi ambayo pia inawakabili mastaa wengine wa bongo movie na watu maarufu..


=================== 
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ametembelea na kuzindua nyumba ya wahudumu wa afya katika kijiji cha Mkungo wilayani Chato mkoani Geita zilizojengwa na taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na Serikali. 

Akizindua nyumba hizo jana, Rais Mkapa aliwasalimia wanachi kwa salam yake ya “mambo” na wananchi kuitika poa” na kuwataka kutunza nyumba hizo na kushirikiana vema na watumishi watakaoshi katika nyumba hizo kisha msafara wake kuondoka na kuelekea Ikulu ndogo iliyopo Chato. 

Mkapa aliingia katika eneo la zahanati hiyo saa sita mchana akiongozana na mkewe, Mama Anna Mkapa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu. Uzinduzi wa nyumba hiyo ni ishara ya kuzindua nyumba nyingine 50 zilizopo katika mikoa ya Geita, Simuyu na Kagera.

Makabidhiano ya nyumba hizo yanatarajiwa kufanyika leo(Jumatatu July 10) katika uwanja wa mpira wa miguu uliopo Chato mjini hafla itakayohudhuriwa na Rais John Magufuli. 

Ofisa Mahusiano na Mawasiliano wa Mkapa Foundation, Deogratius Rimoy alisema nyumba 50 zilizojengwa na taasisi hiyo katika mikoa mitatu tofauti zimegharimu kiasi cha Sh 2.5 bilion Alisema lengo la kujenga nyumba hizo ni ili kuboresha huduma za afya vijijini illi watumishi waweze kutoa huduma za afya kwa saa 24. 


=================================













About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search