Breaking News: Mwakyembe afanya 'mazito' BMT.. #share amtumbua Dioniz Malinzi na 'Convoy' zima..

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) , Dionis Malinzi, ambaye ni ndugu na Rais wa Shirikisho la Soka Jamali Malinzi ametumbuliwa leo na Waziri wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Mwakyembe kufuatia agizo la Waziri Mkuu


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimtaka Waziri Mwakyembe kupitia baraza hilo na kulitathimini hivyo baada ya kulipitia na kutathimini amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti wa baraza hilo.



"Kwa mamlaka niliyopewa na sheria ya BMT Na. 12 ya 1967, nimesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe wote wa BMT"- Dkt.Harrison Mwakyembe

Kwa mujibu wa Waziri Mwakyembe amesema kuwa Sekretarieti ya Baraza la Michezo Tanzania litaendelea na kazi kwa kushirikiana na serikali wakati mchakato wa kuteua mwenyekiti mpya wa baraza hilo ukiendelea..





About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search