Breaking News!! AY na MwanaFA 'waigaragaza' Tigo Mahakama ya Rufaa.. sasa kulamba Bilioni 2.1 fidia.. #share..
Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na kampuni ya Tigo kupinga kuwalipa wasanii AY na MwanaFA Tshs 2,185,000,000 kwa kutumia nyimbo zao bila kulipa.
Wakili Albert Msando ambaye anawakilisha wasanii hao amesema huu ni ushindi muhimu kwa sanaa ya Tanzania.
![]() |
Wanamuzi Ay na MwanaFA katika pozi. |
Amenukuliwa akisema "ni haki yao kulipwa kwa sababu ni kazi zao ambazo zinalindwa kisheria".
Mdau maarufu wa kwenye tasnia ya Bongo Movie na Bongo fleva, John Seka, akiposti ujumbe mrefu kupitia akauti yake ya FB amempongeza 'Wakili Msomi' Albert Msando kwa kutetea haki ya wasanii hao, akisema ni njia ya mfano kwa wasanii 'chipukizi' wanaoporwa haki zao..
No comments:
Post a Comment