Trending News: Wakili Fatma Karume afunguka ya Lissu kupelekwa Central.. #share

News Flash.. Taarifa Mpya kabisa iliyopatikana mchana huu kupitia Afisa habari wa CHADEMA ni kwamba Polisi wamemchukua Tundu Lissu kutoka kituo kikuu cha polisi na wanaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kupekuliwa, ingawa haijajulikana hasa upekuzi huo unahusu nini...
-----------------------------------------
Taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa Tundu Lissu bado anashikiliwa kituoni hapo na jitihada za mawakili wa Chadema kukamilisha Taratibu za dhamana zinaendelea.. 
Fred Kihwelu, akiongea na waandishi wa habari ametonya kuwa hawajajua kama mtuhumiwa wao atapandishwa kizimbani ama laa.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Mwanansheria msomi Fatma Karume alieongea kuhusu muendelezo wa shauri hilo, amesema  wanaandaa waraka maalum kuiomba Mahakama Kuu kumfikisha Lissu Mahakamani haraka kwa kosa analotuhumiwa nalo.
======================
Wakili mahiri kwenye tasnia ya Sheria Bi Fatma Karume akisisitiza jambo.
HAPO AWALI: Wakili Karume alisema polisi walikataa kumpa dhamana mteja wake jana jioni mara baada ya kukamatwa akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.
Karume amesema baada ya kufikishwa polisi, Lissu alitakiwa kuandika maelezo na kupewa onyo kwa kosa la uchochezi.

“Lakini cha ajabu mpaka sasa hivi hatujaambiwa Lissu kamchochea nani, kosa la uchochezi lazima lilete madhara au uhalifu kwa wengine na ni lazima liwe la uhalifu.” Amesema

Amesema hata walipouliza nani anayeweza kuruhusu mteja wake apate dhamana hiyo waliambiwa imezuiwa kwa amri kutoka juu.

Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, (TLS) alikuwa akielekea Kigali, Rwanda, katika mkutano wa wanasheria wa Afrika - Credit mpekuzi huru


Karume amesema uchochezi lazima liwe ni jambo la uhalifu na mpaka sasa polisi hawajamwambia Lissu aina hiyo ya uchochezi.

“Hili ni jambo la kisiasa, Lissu amezuiwa kwenda kwenye mkutano wa wanasheria wa Afrika, jambo hilo linawafanya hata wanasheria wote wa Afrika kujua mwenzao kakamatwa na Serikali,” amesema.

Kwa mujibu wa Karume, Lissu amewapa ujumbe Watanzania akisema Aluta Continua, na kuwa yupo sawa.
============================
Matukio360 ipo kukuhabarisha, tunaendelea kufuatilia yanayojiri kutoka vyanzo vya kuaminika, endelea kuwa nasi karibu yako..

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search