Breaking News: Chadema yapaza sauti kutaka Dk. Mashinji na wenzake waachiliwe haraka.. #share

SEKRETARIETI ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Makao Makuu katika kikao chake cha leo imetoa maazimio manne,
likiwemo la kutaka Katibu Mkuu wake, Dk Vicent Mashinji na viongozi wengine 10
waliokamatwa siku mbili zilizopita kuachiwa huru mara moja kabla hakijachukua
hatua zaidi.
Katika taarifa ya chama hicho
iliyotolewa na Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano, Tumaini Makene, Chadema
kimetaka Dk Mashinji na wenzake kuachiwa kabla ya hatua nyingine
hazijachukuliwa kulinda uhuru na haki za kikatiba na kisiasa zilizoko kwa
mujibu wa sheria za nchi.
“Iwapo kesho Jumatatu mamlaka
hizo hazijamwachia huru Dk Mashinji na viongozi 10, chama kupitia kwa mwanasheria
Mkuu wake kitatangaza maamuzi yatakayochukuliwa kwenye mkutano na waandishi wa habari
utakaofanyika hiyo kesho,” alisema Makene.
“Katika hatua ya sasa Sekretarieti
pia imeelekeza kwa haraka mawakili wa Chama kusimamia kesi dhidi ya Katibu Mkuu
na Viongozi wengine kuhakikisha kuwa masuala ya kisheria yanafuatwa na haki
kutendeka. Kwa sasa jambo hilo litasimamiwa na Wakili msomi Edson Mbogoro.”
Amesema aidha, Sekretarieti imemteua
Katibu ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emanuel Masonga kukaimu kazi za Kanda
ya Kusini wakati ambao Mwenyekiti na Katibu wa Kanda hiyo wakiwa mahabusu.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment