bREAKING nEWS: Kamati kuu Chadema yatoka mafichoni na vipaumbele 'mbadala'.. Mbowe 'amwaga povu' Ubinafsishaji na Pembejeo.. #share

Baada ya kujikita mafichoni kwa masaa zaidi ya 48, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Mwenyekiti wake wa Taifa, Freeman Mbowe imekutana na Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika Dar es Salaam na kuweka mikakati...



Katika mkutano huo, Mbowe ametoa taarifa ya maazimio na mikakati yake kama chama baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kukutana kwa siku mbili mfululizo kuanzia Julai 29 hadi 30, 2017 katika mkutano wa aina yake uliofanyika katika Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, kamati ilifanikiwa kujadili mambo mbalimbali na kufikia maazimio na hatua za kuchukua katika ajenda zao. Katika Mkutano huo, Mbowe ameitaka serikali kutokurupuka katika suala zima la kudai haki ya rasilimali zetu ingawa ni wajibu wetu kama nchi,.. akitahadharisha juu madhara makubwa yanayoweza kutokea katika uchumi wa Taifa, endapo mikakati thabiti na endelevu haitawekwa.

Kamati pia ilijadili suala la pembejeo za kilimo kutowafikia walengwa kwa muda muafaka hivyo kudumaza hali ya usalama wa chakula,.. akihusisha moja kwa moja usalama wa chakula huchangia moja kwa moja usalama wa Taifa husika.. "Hatuchukii mapambano ya kutafuta haki kwenye rasilimali zetu lakini ufanyike utafiti wa kutosha.." alisema Mbowe.

"Hakuna mfanyabiashara duniani ambaye atapewa kitega uchumi ambacho kinamuongezea faida akaamua kukifunga sababu anaichukia TZ," amesema Mbowe akikazia kauli yake kwamba serikali imeshindwa kuwajali wawekezaji, jambo ambalo limesababisha kudumaa kwa sekta ya viwanda na kilimo nchini huku akiitaka Serikali itoe hadharani mpango wake wa muda mfupi kuokoa hali yetu ya kiuchumi.


Mbowe ameongeza kusema takwimu zitolewazo na taasisi husika tunaziamini kwa kuwa zinatolewa na Taasisi kubwa kabisa ya BOT, lakini lazima kuwepo na uwiano unaoonyesha uhalisia kwenye mifuko ya raia wa kawaida waliowengi. "Tutaambiwa uchumi unakua, lakini mbona umasikini unaongezeka?!!, Alishangaa Mwenyekiti huyo wa chama kikubwa kabisa cha upinzani na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni. "...Uchumi unakua mifukoni mwa wale walioko kwenye sekta ambazo zinakua sio kilimo" alisema.


Katika kuelezea nini kifanyike kutukwamua hapa tulipo, Mbowe ameitaka kujikita kujenga mazingira wezeshi katika sekta za kibenki, nafuu ya pembejeo kwa wakulima, na uwekezaji katika sekta ya viwanda, teknolojia na demokrasia.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search