PIGO JENGINE UCHAGUZI MKUU KENYA: Chris Musando wa IEBC auawa kikatili baada ya kutekwa nyara #SHARE

OFISA wa cheo cha juu wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC), ambaye alitoweka Ijumaa ya wiki iliyopita amepatikana akiwa amefariki dunia.


Chris Musando ambaye ni meneja wa masuala ya teknolojia wa IEBC, alipatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhia maiti mjini hapa.

Inadaiwa kuwa, Musando kwa mara ya mwisho aliwasiliana Jumamosi majira ya saa tisa alfajiri kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na mmoja wa wafanyakazi wenzake.

Kisa hiki kinatokea ikiwa imesalia wiki moja, kabla ya uchaguzi mkuu nchini ambao utafanyika Agosti 8.

Polisi wanasema mwili wa ofisa huyo pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la kikuyu lililo vitongoji vya mji wa Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.

Musando alikuwa akihusika na usambazaji wa vifaa vyaa eletroniki, ambavyo vingetumiwa kutambua wapiga kura na kwa upeperushaji wa matokeo wakati wa uchaguzi mkuu wiki ijayo.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search