Breaking News: Mzee Lowasa 'alivyopamba' Mazishi ya Marehemu Joseph Nkaissery yanayoendelea muda huu Jijini Nairobi.. #share..
Tofauti na ilivyo kawaida wakati huu wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazoendelea zinazotawaliwa na purikushani za hapa na pale,.. hali ya huzuni na utulivu imetawala Jijini Nairobi Nchini Kenya leo kunakofanyika Mazishi ya Kitaifa ya Mwanasiasa Mkongwe na Waziri wa Mambo ya Kiusalama wa Ndani wa Kenya Mwendazake Joseph Nkaissery.
Haya ni Mazishi ya kipekee kufanyika katika siku zaribuni ukizingatia historia ya Mwendazake Nkaisery ambae kabla kuteuliwa kwenye Baraza la Waziri katika Serikali ya Jubilee ya Uhuru Kenyatta, alikuwa mfuasi 'gogo' wa Siasa za Upinzani hususan kambi ya Mgombea urais wa Kenya katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Zamani Bw. Raila Odinga..
Miongoni mwa waliohudhuria kutoka nje ya Kenya ni pamoja na Mzee Edward Lowasa kutoka kambi ya Upinzani ambae kama ilivyo kwa Odinga, nae amewahi kuwa Waziri Mkuu katika awamu iliyopita ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete..
Matukio360 imefanikiwa kupata picha kadhaa ya yanayojiri katika mazishi hayo,.. endelea kuwa nasi tuendelee kukujuza..
No comments:
Post a Comment