Bad News!! Matokeo ya kidato cha Sita (6) Yazua Kizaa-zaa Kwa Shule ya Alliance Girls ya Jijini Mwanza.. NECTA yaipiga 'kufuli mazima'.. share...

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limeifungia shule ya sekondari ya Alliance Girls ya Mwanza kuwa kituo cha mitihani kutokana na ukiukwaji wa kanuni za mitihani ikiwemo udanganyifu. NECTA imeagiza kamati ya uendeshaji wa mitihani ya mkoani Mwanza kuwatafutia watahiniwa wa shule hiyo kituo kingine cha kufanyia mitihani.

Akizungumzia udanganyifu uliobainika kwenye shule hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema wakati wa mtihani wa Biology 1, mtahiniwa S4836/0502 wa shule hiyo alikamatwa akiwa na karatasi yenye ‘notes’, ambayo baada ya kukamatwa iliunganishwa na maelezo ya mashahidi, maelezo ya mtahiniwa kukiri kosa na karatasi ya kujibia mtihani ya mtahiniwa ambapo vyote viliwekwa kwenye bahasha.
Dkt. Msonde ambaye alikuwa akitangaza rasmi matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2017, amesema katika hali ya kushangaza, bahasha husika ilipofunguliwa wakati wa usahihishaji, ilibainika kuwa vielelezeo vyote vilikuwa vimeondolewa.
Msonde ameendelea kusema baada ya uchunguzi kufanyika, ilibainika kuwa wasimamizi wa mtihani na askari aliyekuwa analinda kituo hicho walifungua bahasha na kuondoa vielelezo vyote na kisha kuifunga upya bahasha ile.
Amesema uchunguzi zaidi ulibaini kuwa mmiliki wa shule hiyo pamoja na mwalimu mkuu walihusika katika tukio hilo, hivyo kutokana na shule hiyo kupewa onyo mara kadhaa, Baraza hilo limeaua kutumia mamlaka yake kukifungia hadi litakapoamua vinginevyo.


 Bofya hapa chini kama ulipitwa na matokeo ya form six..

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokoe ya kidato cha sita.  Bonyeza HAPA kufatilia matokea ya shule zote Tanzania


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search