TOP NEWS!! TRA yataja idadi ya Vituo ilivyovifungia jana na leo kwa kukwepa kutumia mashine za EFD's .. #share..

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imevifungia jumla ya vituo vya mafuta 71 katika jiji la Dar es Salaam kwa kushindwa kutoa risiti za EFD wakati wa kutoa hduma hiyo.
Miongoni mwa vituo hivyo  28 vipo wilaya ya Kinondoni, 31 Ilala na 12 Temeke. Hata hivyo vituo 52 vimeonyesha ushirikiano kwa TRA kwa kuanza kufuata taratibu na muda wowote vinaweza kufunguliwa endapo itathibika wametimiza masharti.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo amesema  si lengo la TRA kuwaumiza wananchi au kuwasumbua wafanyabiashara bali sheria na taratibu zinapaswa kuzingatiwa.

“Tunaomba wananchi wawe wavumilivu katika kipindi hiki ambacho tunataka sharia na taratibu zifuatwe kwa wafanyabiashara kutumia risiti za EFD kama ilivyoanishwa kisheria na kutangazwa bungeni,”

Aidha Kayombo amewataka wafanyabiashara kutoa ushirikiano kwa kutafuta mashine hizo kwani ndiyo utaratibu unatakiwa kufuatwa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search