bREAKING nEWS:: Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetaja majina ya Wabunge wapya CUF, kujaza nafasi za Wabunge 'waliokaangwa' na Profesa Lipumba... #share

Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imetangaza majina ya wabunge 8 wa CUF ambao imewateua kuchukua nafasi za Wabunge wengine 8 waliovuliwa uanachama kwa sababu za kinidhamu na usaliti katika chama.


Hatua hii ya Tume imekuja siku moja tu tokea Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kuridhia kufukuzwa uanachama kwa Wabunge hao, hatua ambayo ni dhahiri imewanyima sifa na fursa ya kuendelea kulitumikia Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania katika nafasi zao.

Katika nakala ya Uteuzi huo kutoka tume ya Uchaguzi (Nec), na ambayo Matukio imepata nakala yake, umewataja Wabunge wapya walioteuliwa ni pamoja na:

Ndugu Rukia Ahmed Kassim

Ndugu Shamsia Aziz Mtamba

Ndugu Kiza Hussein Mayeye

Ndugu Zainab Mndolwa Amir

Ndugu Hindu Hamis Mwenda

Ndugu Sonia Jumaa Magogo

Ndugu Alfredina Apolinary Kahigi na Bi Nuru Awadh Bafadhili.




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search