gOOD nEWS: Kutoka Kampala International University(KIU); sasa ni Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania (KiuT).. #share

Bado kukiwa na sintofahamu kubwa na vilio vingi kutokana na maamuzi ya TCU kufungia kufanya udahili kwa vyuo vikuu zaidi ya 19 nchini, hali imekuwa tofauti kwa chuo kikuu kilichoandamwa na minong'ono mingi kuhusiana na ubora wake cha Kampala International University (KIU)



Katika kikao chake cha 76 kilichokaa tarehe July 12 mwaka huu, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeidhinisha maombi ya Chuo cha Kikuu hicho ya kukipandisha hadhi kutoka chuo cha Kimataifa hadi Chuo Kikuu cha Kimataifa(Kiu-DCC) na sasa kitajulikana kama Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania (KiuT).

Taarifa iliyotolewa na Profesa Eleuther Mwageni chuo hicho jana imeeleza kuwa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imekubali maombi hayo miongoni mwa maazimio mengine ikiwa ni pamoja na mapitio ya mapendekezo ya Kamati ya Usaili (Accreditation Committee) ya TCU dhidi ya ombi la uongozi wa Kiu-DCC kwa ajili ya kubadili jina..


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search