EXCLUSIVE: Startimes watarusha moja kwa moja Michuano ya Kirafiki ya Mabingwa inayotambuliwa na FIFA... #share..
KAMPUNI ya StarTimes inataarajia kuonyesha michuano ya kombe la kimataifa ya kirafiki ya kimataifa (ICC) itakayofanyika katika nchi tatu tofauti ikiwa ni pamoja na Amerika, Singapore, na China baada ya kupata haki hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo Juma Suluhu, alisema michuano hiyo itarushwa kupitia cheneli tano za michezo zilizopo katika king’amuzi hicho.

Aidha alisema kuwa mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu duniani bila shaka watafurahia mashindano hayo ambapo katika nchi ya amaerika watawashuhudia miamba wawili wa soka ambao ni Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona.
Alieleza si nyota hao tu pekee watakaoshuhudiwa katika ushindani bali kutakuwepo na wengine wakiwemo wachezaji baadhi ya ambao waliokuwemo ndani ya 20 bora katika tuzo za 20 za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) za mwaka jana ambapo alifafanua kuwa timu shiriki zinatumia kujiandaa na ligi zao msimu ujao.
"Ni ushindani mwingine katika soka ya dunia, StarTimes inakuletea baadhi ya timu bora na wachezaji bora katika kila mchezo mmoja. Kutakuwa na mechi 18 zinazoshirikisha klabu 14 katika maeneo 15 katika nchi tatu. Hakuna kitu bora zaidi kuliko hicho. "Alisema Juma.
Juma elisema kwamaba soka ni mchezo unaopendwa zaidi Afrika, kutokana na hali hiyo wameamua kuomba haki ya kurusha mashindano hayo moja kwa moja.
Alibainisha kwamba mchezo wa kwanza utakaoonyeshwa utachezwa kwenye uwanja wa Tianhe, Guangzhou China Julai 18 ambao utakuwa kati ya EC Milan vs Borussia Dortmund.
"Tunafurahi kuwa wateja wetu wanaopenda mpira wa miguu katika bara hilo wataendelea kufurahia soka zuri hata wakati huu wakati ligi nyingi kote ulimwenguni zimeisha. Ni heshima kuleta uzoefu huu wa kusisimua katika nyumba za watanzania "alisema Juma.
Baadhi ya timu zitakazo shiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Manchester United, Chelsea, EC Milan, Borussia Dortmund, Bayern munich, Real Madrid na Barcelona.

No comments:
Post a Comment