TETESI : Uhamisho majira ya Kiangazi na Tour the World... #share

Mchezaji nyota Mjerumani Mesut Ozil, amesema yuko tayari kubakia klabuni Arsenal na anatarajia kusaini mkataba mpya na wapiga bunduki hao wa jiji la London kumalizia mkataba wake wa mwaka mmoja, endapo tu kama maboss wake hao wataridhia matakwa yake ya kitita cha Pauni 350,000 kwa wiki.. (Daily Mail)



Klabu ya Real Madrid imemjumuisha Alvaro Morata kikosini katika ziara ya maandalizi ya klabu hiyo nchini Marekani.. Mshambuliaji huyo kutoka klabu ya Chealsea mwenye umri wa miaka 24 amepania kuwaonyesha Klabu ya Manchester kile ambacho wangefaidi endapo wangefanikiwa kumpandia dau..
Klabu ya Man U na real madrid zinataraji kushea kambi ya mazoezi nchini humo ikiwa ni muendelezo wa ziara za maandalizi za tour the world..(ESPN)


Bosi wa West Brom Tony Pulis amepania kuwavuta wachezaji wawili wa Manchester United Chris Smalling na Phil Jones, ambao wote wawili wamebakiza mkataba wa miaka miwili kuondoka klabuni hapo. Gazeti la the Mirror limemnukuu Tony Pulis akisema Smalling (27) na Phil (25) si wachezaji wa kuwaacha nyuma.

Klabu ya Everton imenawa mikono kwa Mholanzi Jairo Riedewald, baada ya kuzidiwa kete na Crystal Palace ambayo imeingia makubaliano ya moja kwa moja na klabu yake ya Ajax kwa mlinzi huyo kinda mwenye miaka 20 (Telegraph)

Mlinda Mlango wa klabu ya Brighton & Hove Albion Christian Walton amesainiana kujiunga na klabu ya Wigan. Mchezaji huyo kinda mwenye umri wa miaka 21 anatarajia kukamilisha deal lake la mkataba mpya wa mkopo wa miaka minne na hiyo changa katika Ligi kuu ya Uingereza..

Wabashiri wa masuala ya soka wamekata ‘rada’ za klabu ya Manchester City kumnyakua Alexis Sanchez kutoka klabu ya Arsenal.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa akihusishwa na tetesi za kuihama Emirates na kuhamia Manchester city, lakini kwa mshangao ado anaonekana katika matukio ya uzinduzi wa kikosi cha the Gunners. (Manchester Evening News)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search