Good News: PBPA yasema Meli 7 njiani kuingiza mafuta nchini kwa matumizi ya Mwezi wa Tisa...;#share
WAKALA wa Uigizaji Mafuta kutoka nje ya nchini (PBPA)
wamesema takribani meli 7 zinatarajia kuingiza mafuta nchini kwa ajili ya
matumizi ya mwezi wa tisa.
Katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa (PBPA),Modestus Lumato
akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kwa ajili ya kutangaza
tenda ya kampuni itayoleta mafuta kutoka nje ya nchi leo jiji Dar es Salaam,
Pia,(PBPA) imesema wafanyabiashara wa mafuta nchini
wameridhishwa na Bajeti ya serikali ya mwaka 2017-2018 kutokana na kutoa fursa
ya kuyarusu magali mengi kuingia barabarani jambo wanalodai litapelekea
matumizi ya mafuta kuongezeka.
Hayo yameelezwa leo Jijini dare s Salaam,na Kaimu Mkurugenzi
wa (PBPA),Modestus Lumato wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwa
ajili ya kuitangaza kampuni ambayo iliyoshinda tenda ya kuagiza mafuta toka nje
ya nchini.
Amesema kati ya hizo meli hizo, meli tatu zitakuwa na mafuta
ya Diseli,tatu zikiwa na mafuta ya Petroli huko moja ikiwa ni mafuta Taa.
Amesema kwa sasa zimejitokeza kampuni 7 kwenye kuwania tenda
ya uigizaji mafuta hayo kuyaleta hapa nchini huku ikitakiwa kampuni moja .
‘Katika kampuni hizi saba kampuni sita kutoka nje ya nchi
huku kampuni moja kutoka hapa nchini,sababu inayopekelekea kwa kampuni za ndani
kushindwa kujitokeza kwa wingi kunatokana na uigizaji huu kuitaji fedha nyingi
jambo ambalo linawashinda kampuni za ndani kuwa na mtaji mdogo’amesema
Lumato.
Lumato amebainisha kuwa kwa sasa mahitaji ya mafuta yameongezeka
kutokana na wafanyabishara kuridhishwa na bajeti ya serikali 2017-2018
iliyopitishwa na Bunge.
‘‘kwenye mwezi wa sita wafanyabiashara walipunguza wingi wa
uigizaji wa mafuta kutokana na kusubiri bajeti ya serikali,lakini
kwa sasa bajeti imepita na imetoa ruhusa kwa magari mengi kuingia barabarani
kwa kutoa tozo za kodi zilizokuwa zinazuia magari kuingia barabarani ,kwa sasa
magari mengi yataingia barabarani na kupelekea mafuta mengi kutumika”amesema
Lumato.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment