nEWS: Jeshi la Polisi 'Mkoani Temeke' lashikilia 16 na wazazi wao kwa utoro mashuleni.. #share

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke limewatia mbaroni wanafunzi 16 kwa utoro shuleni katika msako wa kuwabaini wakhalifu.

Halikadhalika linawashikilia Wazazi 10 wa miungoni wa wanafunzi hao kwa kushindwa kuhudhulisha watoto hao shuleni.

Kamanda Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke,Gilles Muroto akiwaonyesha watoto watoro na wazazi wao kwa waandishi wa habari.
Akizungumza Dar es Salaam leo Kamanda Msaidizi Mwandamizi,Gilles Muroto,alisema kutokana baadhi ya wanafunzi kutohudhuria shuleni hali ambayo wengi wao wamekuwa wakijiingiza katika matukio ya uhalifu madawa ya kulevya kama bhangi.

“Tumewakamata wanafunzi 16 pamoja na wazazi 10 wao ili kutekeleza ukubwa wa zoezi hili ambalo ni endelevu na kama mzazi ni wajibu wake kujua na kufatilia mwenendo na mahudhurio ya watoto wao katika kupata elimu na kuacha kuzunguka mitaani wakati wa shule,”alisema Muroto.

Alisema wananchi wote waliokuwa katika Mkoa wa Kipolisi Temeke watoke katika wimbi la watoto kuacha utoro ili kuwaepusha kutumbukia kwenye wimbi la madawa ya kulevya,ukabaji na matukio yenye majina mabaya kama Panya Road,Black American na Machizi. 

Muroto ,alieleza kuwa kama mzazi ni wajibu wa kujua mwenendo wa mtoto ili asiweze kujikita katika matukio ya uhalifu hivyo Kifungu cha Sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 kinachoeleza kuwa ni kosa kwa mlezi au mzazi kukiuka kwa makusudi na kuzembea kutoa huduma ya chakula, malazi,matibabu na elimu ya mtoto.

“Jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Temeke linawashikilia wazazi 10 kwa kutofatilia mwendo watoto wao pamoja na wanafunzi 16 na tutawafikisha mahakamani ili kutokomeza utoro endelevu katika mkoa wa kipolisi ,”alisema Muroto.

Kwa upande wa mmoja wa wazazi,Josepheni John alisema naiomba Serikali inisaidie tabu ninayoipata kwa mtoto juma ni kubwa kutokana na mtoto huyo kuwa mtoro.

“Mtoto wangu haachi utoro mimi kama mzazi nakamatwa kwa ajili yake hali ambayo mtoto wangu angekuwa ameshamaliza shule muda mrefu ila kwa utoro wake hadi leo yupo darasa la tano,”alisema Josepheni. 

Aidha Jeshi hilo pia linawashikilia watuhumiwa 38 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 25 kwa kukamatwa na makosa mbalimbali ya uhalifu nyakati za usiku.



Dalila Sharif.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search