Good News!! Waziri Mkuu Majaliwa aagiza Milioni 900 za ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ziende kwenye ujenzi wa Hospitali.. #share

Waziri mkuu Kasim Majaliwa ameuagiza uongozi wa halmashauri ya mji wa Tunduma wilayani Momba, kutumia milioni 900 zilizotengwa kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya halmashauri, zitumike kuanzisha ujenzi wa hospitali.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika moja ya Mikutano yake ya hadhara




Waziri mkuu ametoa agizo hilo jana jioni Ijumaa Julai 21, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Tunduma iliyopo mkoani Songwe.

“Kwa kuwa afya ni jambo muhimu katika utekelezaji wa kauli mbiu ya rais Dkt. John Magufuli ya 'Hapa Kazi Tu' hivyo naagiza fedha zilizotengwa kuanza ujenzi wa ofisi zitumike katika ujenzi wa hospitali.” alisema Majaliwa.

Waziri mkuu amewataka viongozi wa halmashauri hiyo kuongezea shilingi milioni 126 katika ujenzi huo, fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya kuwafidia wamiliki wa eneo lililotengwa awali kwa ajili ya kujenga hospitali, ambapo aliwataka watafute eneo lisilohitaji fidia.

Waziri mkuu pia ameuagiza uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuandaa ramani kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo na kuhusu suala la ujenzi wa ofisi serikali italishughulikia


Na: Ally Bakari

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search