Breaking news: Picha 4 za Tukio baya la ajali Yombo; lasababisha vifo vya watu wawili na makumi ya abiria kujeruhiwa vibaya.. #share

Kumeripotiwa tukio baya la ajali iliyotokea asubuhi ya leo ambapo watu kadhaa wamejeruhiwa na wengineo vibaya sana baada ya basi la abiria maarufu Daladala kuigonga Treni katika eneo maarufu la Tandika Relini.

Daladala hiyo aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T427 BQZ linalofanya safari zake kati ya Buza na Gerezani limekigonga kichwa cha treni kwenye makutano ya treni ya Devis Kona

Majeruhi wengi waliokuwa kwenye daladala wamekimbizwa hospitali, na hadi sasa, watu wawili wameripotiwa kufariki kufuatia mkasa huo.. 

Matukio360 inaendelea kuwapa updates kutoka eneo la tukio kabla zitakavyojiri.. usibanduke kwenye uzi huu..






kama hii ilikupita nayo..

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search