Good News: Wizara ya Afya yatangaza nafasi 3152 za ajira.. #share
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto imetangaza nafasi za ajira 3152 kwa wahitimu katika kada mbalimbali za
afya nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa kitengo
cha mawasiliano serikalini-Afya, Nsachris Mwamaja, inaeleza kuwa ina jukumu la
kuwapangia vituo vya kazi waombaji wenye sifa
kwa mujibu wa waraka wa maendeleo
ya utumishi namba moja wa mwaka 2009 kuhusu miundo ya watumishi wa kada chini
ya wizara hiyo.
Miongoni mwa nafasi hizo, zipo za wauguzi wa daraja la
kwanza na la pili, wapo wataalamu wa maabara, wanateknolojia na wataalamu wa
lishe.
“Sifa za muombaji; awe raia wa Tanzania, awe na umri
usiozidi miaka 45, asiwe mwajiriwa wa serikalini, hospitali za mashirika ya
dini ambaye mshahara wake unalipwa na serikali na asiwe amewahi kufanya kazi
serikalini na kuacha kazi,” ilieleza taarifa hiyo.
Na: Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment