GOOD News!! Wizara ya Madini 'yawashusha pumzi' watumishi wa 'TMAA' #share..

WIZARA ya Nishati na Mdaini imesema kwamba watumishi waliokuwa wafanyakazi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Ofisi za Madini za Kanda ambao hawana tuhuma zozote wataendelea na ajira zao chini ya Kamishna wa Madini.

Prof. James Mdoe, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini..
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Saalaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa James Mdoe akizungumza na waandishi wa habari, alisema hiyo ni kutokana na wafanyakazi hao kuwa ni watumishi wa Serikali katika wizara ya Nishati na Madini.

“Pamoja na kufutwa kwa TMAA na Ofisi zake za Madini za Kanda, watumishi waliokuwa wanafanyakazi kwenye Taasisi/Ofisi hizo ambao hawana tuhuma ziozote wataendelea na ajira zao,” alisema Profesa Mdoe.

Aidha ametaja majukumu yao ambayo watayatekeleza katika wizara hiyo kuwa ni pamoja na kukusanya maduhuli ya serikali yanayotokana na madini ya Ujenzi na madini ya viwandani na pia kuhakiki vocha za malipo ya mrabaha, kukagua migodi, ya wachimbaji wakubwa, wachimbaji wa kati na wachimbaji wadogo.

Mengine ni kukagua miradi yote ya wazalishaji dhahabu kutokana na marudio kupitia teknolojia ya vat leaching, kukagua maeneo ya viwanja vya ndege, bandari na mipakani ili kudhibiti utoroshwaji wa madini, kupokea malipo ya tozo mbalimbali kwa mujibu wa sheria ya madini na kutoa hudumu za ugani kwa wachimbaji wadogo na kusimamia masuala yote ya usalama mogodini.

Amesema katika kipindi hiki cha mpito kabla ya Tume ya Madini haijaundwa, shughuli zote zitafanywa chini ya usimamizi wa kamishna wa madini.

Amebainisha pia katika kipindi hiki cha mpito, serikali imesimamisha utoaji wa leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini hadi hapo Tume ya Madini itakapokuwa imeundwa na kuanza kazi rasmi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search