hABARI uPDATES: Esther Bulaya 'kampaa - kampaa tena..' 'Tyson aambulia kichapo kingine Mahakamani.. #share

Mahakama ya Rufani imetupia mbali rufaa iliyokatwa na wapiga kura 4 wa Jimbo la Bunda Mjini kupinga ushindi wa Mbunge, Esther Bulaya.


Baada ya ushindi huo Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya ameandika ujumbe huu: Wana Bunda wameshinda tena na tena,asante Mungu

Shauri hilo lilifunguliwa na Magambo Masato na wenzake wanne, wakiiomba mahakama kutengua matokeo yaliyompa ushindi mbunge Ester Bulaya9CHADEMA), aliyekuwa kada wa CCM kabla ya kuhamia Chadema.

Miongoni mwa madai ya msingi ya walalamikaji yaliyowasilishwa mahakamni wakiwakilishwa na mawakili wawili, Constatine Mutalemwa na Denis Kahangwa, walidai aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Stephen Wasira alikataliwa ombi la kuhesabu wala kuhakiki kura baadhi ya vituo, kuwapo mianya ya rushwa na kunyimwa haki yao ya kuchagua - JF

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search