KOCHA wa Filamu za Bongo "Claude 112" ametuletea 'Usijisahau'.. ni baada ya kujichimbia Sweden kwa miaka 4..
MSANII wa Bongo-movie, Issa Mussa a.k.a “Claude 112” amewasili nchini hivi karibuni akitokea Stockholm, Sweden alikokuwa amepiga kambi kipindi cha miaka minne(4) na kutinga Ofisi za maelezo, na kuongea mengi juu ya ujio wa filamu yake mpya ya "Usijisahau”
Akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam mchana huu amesema maandalizi ya awali ya kuinadi filamu hiyo ya Usijisahau itakayozinduliwa rasmi kati mwezi wa 10 au 11 mwaka huu yamekamilika.
Claude amesema, filamu ya usijisahau imebeba ujumbe mkubwa na muonekano mpya kwa jamii hasa katika mazingira yaliyochukua yaliyoshutiwa kutoka nchi nyingine ukitofautisha na yaliyozoeleka katika Nchini Tanzania.
“Kila kitu katika muvi hii nimefanyia hukohuko nchini Sweden chini ya kampuni yangu ya AIMUS na nimeshirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu nguli wa hapa nyumbani, kama vile Suleiman Barafu na Wastara Juma,” amesema Claude.
“Kama kawaida ya muvi zangu nyingi, hii pia ina maadili ya kidini kidogo na ina mafundisho mengi mno juu ya maisha ya watu wa jamii yetu nitaisambaza kwa kulingana upepo wa soko la tasnia yetu kwa sasa hivyo tutarajie mazuri kutoka katika movi hii.”
Akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam mchana huu amesema maandalizi ya awali ya kuinadi filamu hiyo ya Usijisahau itakayozinduliwa rasmi kati mwezi wa 10 au 11 mwaka huu yamekamilika.
“Kila kitu katika muvi hii nimefanyia hukohuko nchini Sweden chini ya kampuni yangu ya AIMUS na nimeshirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu nguli wa hapa nyumbani, kama vile Suleiman Barafu na Wastara Juma,” amesema Claude.
“Kama kawaida ya muvi zangu nyingi, hii pia ina maadili ya kidini kidogo na ina mafundisho mengi mno juu ya maisha ya watu wa jamii yetu nitaisambaza kwa kulingana upepo wa soko la tasnia yetu kwa sasa hivyo tutarajie mazuri kutoka katika movi hii.”
Amesema stori nzuri inayozungumzia wanadungu wawili hivyo inamafundisho mazuri na maadili mazuri kwa jamii -
Na Dalila Sharif
No comments:
Post a Comment