Picha 6: Wabunifu wa 'Roboti ya Kitanzania' walivyokabidhiwa Bendera na Naibu Waziri wa Elimu Bi Stella Manyanya.. tayari kwenda kushindana marekani.. #share


NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Stella Manyanya amewataka wanafunzi nchini kujikita katika masomo ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwa ajili ya maisha yao ya badae badala ya kutafuta mimba.


Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakati akiwakabidhi Bendera ya Taifa timu ya wanafunzi saba wanaokwenda nchini Marekani kwa ajili ya mashindano ya maonyesho ya sayansi na teknolojia.

“Yani wewe wenzako wanafanya mambo makubwa kama haya lakini wewe uko bize kuzitafuta mimba, eti nani yuko tayari, uko mtoto ufanye kazi mbili kufikiria mtoto wangu analia nyumbani, halafu ya kufikiria kwamba natakiwa kusoma,” alisema Manyanya.

Aidha amebainisha kuwa ndoto ya Rais John Magufuli ya kufikia uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda haiwezi kufikiwa bila kuwekeza na kufanya vizuri katika eneo ya sayansi na teknolojia ambapo alisema kuwa kwa mwaliko wa wanafunzi hao kwenda kushiriki katika mashindano hayo ni ishara nzuri kwa Taifa.

Ameeleza kwa kusema kwamba vijana wa aina hiyo ndiyo watakao wezesha nchi kufika katika maendeleo ya viwanda na kusema kuwa hilo ni faraja kwa Tanzania

Ameongeza kuwa juhudi za serikali za kuhakikisha wanafunzi wengi wanasoma masomo ya sayansi tayari serikali imekwisha sambaza vifaa mbalimbali vya maabara katika shule za hapa nchini.

Mkuru Shabani kutoka Taasisi ya Wahandisi wanawake (Women Chapter) ambaye ni mwalimu wa wanafunzi hao alisema kuwa katika mashindano hayo watakwenda kuonyesha Roboti waliyotengeneza ambayo kazi yake ni kutenga maji safi na machafu.

Amesema wanakwenda kutokana na mwaliko waliopewa na shirika la Kimarekani la First Globle For Ricognation and Insperation Of Science and Technology ambalo linajihusisha na uhamasishaji wa vijana katika kusoma masomo ya sayansi hususani uhandisi.

Alibainisha kuwa takribani mataifa 70 yatashiriki katika mashindano hayo yaliyopewa heshima kubwa ya kuandaa mkutano wa wahandisi kutoka katika sehemu mbalimbali duniani ambao ndiyo watakao fungua mashindano hayo.

Naye Kepteni wa timu hiyo Raymond Benedict amemhakikishia Naibu Waziri kuwa watarudi na ushindi kutokana na maandalizi waliofanya.


Robbot ya Kisasa iliyobuniwa na wanafunzi wa Kitanzania

Mbunifu akitest robot mbele ya Mhe. Naibu Waziri Manyanya

Mmoja wa wabunifu akitoa maelezo ya namna robbot waliyoibuni inavyofanya kazi


Mhe. Naibu waziri akiongea na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani 

Picha ya pamoja ya wabunifu wetu baada ya kuagwa na Mhe. Naibu waziri

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search