nEWS:: CAG aipa 'Hati Safi' UKAWA jijini Dar es Salam,.. afichua DDC nako kwanukia ufisadi...#share
UTENDAJI wa uongozi mpya wa ya Jiji la Dar es Salaam, umeibua uwezekano wa kufanyika kwa ufisadi mkubwa katika mapato ya Shirika la Maendeleo jijini Da es Salaam (DDC).
“Mtakumbuka pale DDC tulikuwa tunakusanya Sh. milioni 50 sasa tunakusanya Sh. milioni 750, pia Benjamini Mkapa tulikuwa tunakusanya takribani Sh. 100,000, lakini kwa sasa tunakusanya hadi Sh. 400,000,” alisema Mwita baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la Madiwani wa jiji jana.
Amesema kutokana na kuongezeka kwa ukusanyaji huo wa mapato, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika ripoti yake ya mwaka 2016/17 aliipatia halmashauri hiyo hati safi.
Ameongeza kuwa kutokana na ongezeko la mapato hayo, wamekata matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za makusanyo hayo, ili zitumike kwa matumizi ya lazima na sahihi yenye tija kwa maendeleo ya wakazi wa Dar es Salaam.
Mwita amesema kutokana na kuongezeka kwa halmashauri nyingine mbili katika jiji hilo ambazo ni Ubungo na Kigamboni, ana mpango wa kupeleka mawakala wa ukusanyaji wa mapato.
Amewataka viongozi wa halamashauri zote za jiji, kuhakikisha wanawatumika wananchi kwa kuwa wao wapo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na kuwashirikisha kwa kila hatua.

No comments:
Post a Comment