Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kesho mgeni rasmi kongamano la wanawake waombolezao....#share
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassani anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Waombelezao Kitaifa
kesho jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Deborah Malassy ambaye
Mratibu wa kongamano hilo wa kwanza kulia akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo kuhusu kongamano la Wanawake Waombelezo Kitaifa.
Hayo yamebeinishwa leo jijini Dar es
Salaam na Mratibu wa Kongamano hilo Deborah Malassy akizungumza na waandishi wa
habari, amesema lengo la kongamano hilo ni kuwajengea uwezo viongozi wanawake
katika kutambua nafasi zao ili kuwawezesha kupata ujasiri wa kuongoza.
“Katika kongamano hili kutakuwa na
utoaji elimu kwa wanawake jinsi ya kujilinda na unyonyaji wa kijinsia, kutoa
elimu ya ukatili wa rushwa ya ngono na kuwapatia elimu ya njia za kujitambua
kiuchumi katika jamii,”amesema Deborah.
Aidha amesema katika kongamano hilo
pia watamuombea Rais John Magufuli ili Mungu ampe nguvu katika kuendelea na
majukumu yake ya kulinda Taifa, kukuza amani na uchumi wa Nchi.
Mchungaji Deborah amewaomba wanawake
kujitokeza katika kongamano hilo ili kuwajengea uwezo wa kiroho, kijamii na
kuunda mitandao ya wanawake mbalimbali kutokana na malengo yanayofanana na
kuwajengea nguvu ya pamoja.
Na
Dalila Sharif
No comments:
Post a Comment