MORNING NEWS: Mama Samia ateta na Bi Mary Robinson Ikulu Jijini Dar es Salaam... Shibuda amuomba JPM amsamehe Ngeleja... #share.. Mawaziri waungana uzinduzi kiwanda cha kisasa cha Viatu Kilimanjaro,.. na "Mnyange Lulu Diva afunguka mambo ya kudekezwa haya.."

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda amemuomba Rais John Magufuli kuwasamehe wale wanaorejesha fedha walizopewa na Mkurugenzi wa kampuni ya VIP Engendering, James Rugemalira ambazo zimetokana na sakata la Escrow. 




Shibuda ameyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja kuwasilisha kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) shilingi milioni 40 alizopewa na Rugemarila. 
Alisifu kitendo cha Ngeleja kurejesha fedha hizo akiwataka wengine waliopata gawio la Escrow kuchukua uamuzi kama huo huku akiwaombea msamaha. “Kwa kitendo chake Ngeleja kutubu, tukubali tusiwe na inda na choyo ila wale wengine nao wakubali kuzirejesha fedha na mheshimiwa Rais awasamehe kama dini zetu zinavyosema, mtu akitubu asamehewe,” alisema Shibuda ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama cha Ada Tadea. James Rugemalira ambaye pia alikuwa na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Mwenyekiti mtendaji wa PAP, Habinder Seth Sigh walifikishwa mahakamani kujibu mashtaka sita ikiwa ni pamoja na uhujumu uchumi - D24
 ===================================

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA IRELAND NA BI. GRACA MACHEL
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Taifa halipo tayari hata kidogo kupokea misaada yenye masharti ambayo hayaendani na mila na desturi za Kitanzania.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari imesema kwamba kauli hiyo imetolewa leo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu wa Ireland, Mary Robinson na Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Craca Machel pamoja na ujumbe walioambatana nao Ikulu- jijini Dar es Salaam.

“Kuna baadhi ya wafadhili wanaisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na bajeti vizuri sana na bila masharti mabaya lakini kuna baadhi ya wafadhili wanaonyesha wazi kuwa wanataka Serikali ikubali masharti yao ambayo yanaenda kinyume na maadili ya taifa kitu ambacho hakiwezekani,” amesema.

Amesema kutokana na changamoto hiyo Serikali itaendelea kusimamia maadili ya Taifa ipasavyo na imeweka mipango na mikakati mizuri kwa ajili ya kuongeza mapato yake ya ndani ili kuondokana na utegemezi kutoka kwa baadhi ya wafadhili ambao baadhi yao wanaahidi kuchangia bajeti kuu ya Serikali lakini mwisho hawafanyi hivyo.

Akizungumzia Kuhusu Sekta ya afya, Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali imeongeza maradufu bajeti yake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 katika sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa viwango vinavyotakiwa nchini.

Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Ireland Mary Robinson pamoja na Mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Graca Machel, Craca Machel waipongeza Serikali kwa jitihada inazozifanya katika uimarishaji wa sekta ya afya nchini na wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha huduma za afya nchini zinaendelea kuboreshwa ipasavyo.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson ambaye pia ni Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Rais huyo Mstaafu aliongozana na Mjumbe mwingine wa Taasisi hiyo Bi. Graca Machel . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson ambaye pia ni Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Rais huyo Mstaafu aliongozana na Mjumbe mwingine wa Taasisi hiyo Bi. Graca Machel . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson pamoja na Bi. Graca Machel ambao ni Wajumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, wengine pichani ni Ujumbe ulioongozana na Viongozi hao pamoja na Wasaidizi wa Makamu wa Rais. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Bi. Graca Machel ambaye aliongozana na Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson kumtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson (kulia) ambaye pia ni Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, kushoto ni Mjumbe wa Taasisi hiyo Bi. Graca Machel mara baada ya kumaliza mazungumzo kwenye ofisi za Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


=============================
Msanii wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma ya Utamu, Lulu Diva amedai katika vigezo ambavyo anavyoangalia wakati wa kuingia kwenye mahusiano ni pamoja na mwanaume mwenye shahuku ya mafanikio lakini pia atakayeweza kumvulia na kuwa msikivu.
Diva huyo anayekuja kwa kasi kwenye 'game' ya bongo ameeleza kuwa licha ya kuhitaji mwanaume mwenye vigezo hivyo, lakini pia anapaswa kujua kwamba Lulu Diva ni msichana mrembo na anayependa sana kudekezwa. “Mpaka mtu awe na mimi kwenye mahusiano kuna vigezo naviangalia. 

Kwanza kabisa nampenda mwanaume smart mind, mtu ambaye ameshika dini anamuheshimu Mungu, pia gentlemen kama hivyo awe ananidekeza awe ananijali, , understanding, passion na Sacrifice," 

Msanii huyo ambaye ni zao la warembo waliokuwa wakipamba nyimbo za wasanii kabla ya kugeukia tasnia ya uimbaji amesema pamoja na kupenda kwake kudekezwa haimaanishi kwamba anababaishwa na vitu vidogo vidogo, La! hasha yeye ni mrembo lakini pia mtafutaji anayejituma -EATV


=======================================




















About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search