Gumzo: Povu la Queen Darleen kuhusu 'kudetishana' na Ali Kiba.. #share..


Cover Foto
======================
Kuhusu #UDAHILI

1.Kwa waliomaliza Cheti na Diploma wanatakiwa kuwasilisha nyaraka zao NACTE ili zihakikiwe(verification) kupitia Link ambayo imetolewa kupitia mtandao wa NACTE baada ya uhakiki huo utapewa #code_namba kulingana na ufaulu wako ambayo ndio itakuwezesha kufanya UDAHILI kwenye chuo kikuu unachokipenda,kumbuka Hakuna chuo kitapokea maombi ya udahili bila code namba hiyo,zoezi limeshaanza na linaendelea Hadi sasa .



2.Kwa waliomaliza Kidato cha Sita maombi UDAHILI kwa mwaka huu Unafanyika moja Kwa moja kupitia chuo na sio TCU kama miaka iliyopita, UDAHILI utaanza tarehe 22.07.2017 hadi 30.08.2017,hivyo mwanafunzi atafanya maombi ya kusoma shahada kupitia chuo anachokipenda, vyuo vikuu vyote vimeshapewa maelekezo kupitia maafisa UDAHILI (admission officers) kupitia mafunzo maalum yaliyoisha tarehe 15.07.2017,Kitu cha muhimu ni kwamba mwanafunzi hatolazimika kusafiri kwenda chuo husika kila kitu kitafanyika kupitia mtandaoni (Online), Anachotakiwa kufanya mwanafunzi ataingia kwenye Website ya chuo utatafuta link ya udahili na kufata taratibu ambazo zimeweka.



Mwanafunzi atajaza taarifa chache Sana ,maana chuo kimewezeshwa kuwa na muingilano Wa mfumo data na NECTA na NACTE, mwanafunzi atajaza taarifa muhimu tu kama vile majina kamili ,index namba zote Hata kama uliwahi ku Reseat zaidi ya mara moja,email na code namba kwa waliomaliza Cheti na Diploma.



Muda uliotengwa ukiisha baada ya tarehe 30.08.2017 hakutakuwa na nyongeza ya muda .


Baada ya hapo majina yatatolewa kwa kila chuo na mwanafunzi aliyedahiliwa atathibitisha usomaji wake kwenye chuo kimoja hata kama jina lake limejitokeza kwa vyuo zaidi ya kimoja.



NB: Maelekezo zaidi yanapatikana kupitia

• www.nacte.go.tz kisha Bofya Award verification

• www.tcu.go.tz kisha Bofya Admission procedures for 2017/18 uzisome kwa umakini na kuzielewa kuepuka kusumbuka dirisha likifunguliwa.


Na: Julian Msacky

_________________________

_________________________


CHAMA cha wapangaji Tanzania kimempongeza Raisi John Magufuli kwa utendaji wake wa kusimamia rasimali za taifa na kuendelea kudumisha amani na upendo kwa watanzania wa jinsia zote.



Hayo yamezungumzwa leo na Katibu mkuu wa chama hicho Ndumey Mukama alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amezungumzia kuhusu kupigania na kueneza ulelewa kuhusu haki za wapangaji.



Amesema kwamba lengo ni kuhakikisha kuwa kuna mahusiano ya kisheria kati ya mpangaji na mpangishaji kupitia mikataba ya upangaji inayojali pande zote mbili na kuwaomba wapangaji kote Tanzania kutambua chama hicho ili kiweze kuwasaidia.



"Pamoja na changamoto nyingi zinazokabili chama chetu tunatoa rai kwa wadau wa kutetea wapangaji ikiwa ni pamoja na kusuluhisha migogoro kati yao na wapangaji pamoja na wakuelemisha wajue haki zao" alisema.



Amesema matarajio ya chama chao ni kuona Serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa sera ya nyumba ambayo itazaa kanuni na taratibu ya upangaji.

Aidha wamelitaka shirika la Nyumba la Taifa kuwa Nyumba zilizotaifishwa tangu mwaka 1971 zikawekwa chini ya msajili wa majumba na baadae kwa kupitia sheria ya bunge liweze kuteua shirika la nyumba la Taifa na kulipa mamlaka ya luziangalia na kuzikarabati.

"Sisi kama chama cha Wapangaji Tanzania tunashauri Msajili wa wa vyama aweke utaratibu wa kutosajili vyama vyingi ili kuepuka migongano katika utekelezaji" alisema.

Hata hivyo alisema wanashauri kuwepo na uwiano katika maswala ya ulipaji wa fidia kati ya mpangishaji kwenye atahari ya nyumba yake mpangaji kwenye upotevu wa mali zake zilizokuwemo ndani ya Nyumba.

Na: Jeymar Makamba
_________________________

_________________________


RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT).

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,Mwenyekiti wa (ALAT) Taifa,Gulamhafeez Mukadamu,anasema kuwa mkutano huo utakaohudhuliwa na mgeni rasmi Rais Magufuli tarehe 19 mwezi wa 9 mwaka huu Mkoani Mbeya wenye malengo makubwa ya kurudisha imani ya wanachama wake. 

Anasema mkutano huo unatarajiwa kuhudhuliwa na wajumbe na washiriki 500, kwa lengo la kurudisha umoja wa kufanya kazi kwa kushirikiana kwa ajili ya Serikali za Mitaa Tanzania katika kuondoa umaskini na kuongeza mafanikio. 

“Alat inamuunga mkono Rais Magufuli kwa juhudi zake katika masuala mbalimbali juu ya nguvu kazi yake katika utendahji bora katika serikali yake na tunashukuru kwa kutupatia kibali kwa ajili ya mkutano huu,”alisema Mukadamu. 

Alisema pia (ALAT) inawatarifu wanachama wake kuanzia tarehe 1mwezi wa 8 mwaka huu ofisi ya Alat itahamishiwa kuelekea makao Makuu Dodoma kwa ajili ya kumuunga mkono Rais. 

Pia ameeleza Kamati ya Utendaji imejipanga vema na kutoa muungozo na ushauri katika kuleta (Alat) katika sura mpya ya kuleta maendeleo ya utendaji kazi wake. 

“Katika kipindi cha mpito kulikuwa hakuna Katibu Mkuu hali ambayo Jumuiya hiyo ilionyesha kuyumba lakini kwa sasa tunashukuru viongozi wa Serikali kwa kutupa ushirikiano mzuri kuteua Katibu Mkuu mwingine katika Jumuiya yetu,”alisema Mukadamu. 

Aidha imewataka wanachama wa Alat waendelee na michango kwa kutoa ushirikiano katika kuendeleza jengo litakalojengwa mkoani Dodoma kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika kutoa fursa mbalimbali kwa viongozi wa Serikali za Mitaa na wadau wengine ili kutatua changamoto na kuondoa umaskini.


Na: Julian Msacky
_________________________

_________________________



MICHUANO ya International Champions Cup 'ICC Cup' 2017 imeendelea tena usiku wa kuamkia Leo kwa mchezo mmoja kupigwa huko nchini Marekani.

Mchezo huo ulikuwa ni wa Manchester Derby ambao ni mahasimu wawili katika jiji moja kati ya Manchester United dhidi ya Manchester City,pambana hilo lilianza saa 11 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki.

Mchezo huo ulimalizika kwa Manchester United kushinda bao 2-0 dhidi ya hasimu wake Manchester City,United walionekana kucheza mpira mzuri zaidi ya wapinzani wake na kupelekea United kushinda mchezo huo ambapo wafungaji wa mchezo huo alikuwa Romelu Lukaku na Marcus Rashford.

Lukaku anazidi kuwa bora katika kikosi cha United kwa maana mpaka sasa tayari ameshafunga magoli 2 katika Mechi tatu ambazo amecheza mshambuliaji huyu wa kibelgiji.

Na: Daniel Shinji Kagawa
_________________________

_________________________

Mfuko moja uliotumika na mwana'Anga Neil Amstrong kukusanya violezi vya mwezi umeuzwa kwa dola milioni 1.8 mjini New York.
Mfuko huo kutoka kwa chombo cha angani Apolo 11 mwaka 1969 ulinunuliwa katika eneo la Sotheyby na mtu asiyejulikana.
Mfuko huo bado una vumbi na mawe madogo madogo kutoka mwezini.

Mnada huo unajiri baada ya mapambano mahakamani kuhusu umiliki wa kifaa hicho cha kipekee kutoka kwa ujumbe wa Apollo 11 ambao ulikuwa katika mikono ya mtu binafsi.
Baada ya chombo hicho cha angani kurudi duniani, vifaa vyote vilipelekwa katika jumba la makumbusho la Smithsonian.
Hatahivyo mfuko huo uliwachwa katika boksi katika kituo cha vyombo vya angani cha Johnson kutokana na makosa ya kihesabu.
Baadaye haukutambulika wakati wa mnada wa serikali, ukiuzwa kwa dola 995 pekee kwa wakili mmoja wa Illinois 2015.
hatahivyo mamlaka inayosimamia vyombo vya angani Nasa ilijarabu kuuchukua mfuko huo, lakini mapema mwaka huu jaji mmoja aliamuru kwamba ulimilikiwa na mnunuzi huyo kimakosa ambaye baadaye ailiupeleka katika mnada huo wa Sutheby.


Bbc - Swahili 
_________________________

_________________________

Kabla Diamond hajakua nyota Tanzania, Ali Kiba na Queen Darleen walikua marafiki wa dhati. Diamond aliponza kutawala kimuziki, Ali Kiba alianza uadui na yeye kisa kilichosababisha kusambaratika kwa uhusiano wake na Queen Darleen ambaye alisimama na kakake.

Ukaribu wa Queen Darleen na Ali Kiba ulichangia kuzuka uvumi kuwa wawili hao walikua wapenzi, madai ambayo dadake Diamond amepinga.

“Sio kweli Alikiba hajawahi kuwa bwana wangu, Ali Kiba ni ndugu yangu na tuna heshimiana sana zaidi ya sana. Unajua mimi watu mpaka leo hawajua mwanamume wangu nani, kwa hiyo hata wewe naweza nikazunguka nawe wiki mbili halafu watasema ni wewe. Ali Kiba ni ndugu kabisa, ni mshikaji wangu na ndivyo ilivyokuwa tunazunguka naye sana. Ikumbuke kipindi kile nilikuwa nazunguna na Ali tayari nilikuwa mjamzito kwa hiyo kwa mantiki hiyo basi yule mtoto angekuwa wa Ali Kiba. Nimeambiwa watu wengi bwana angu hadi Dully Sykes wakati ni ndugu. Kipindi hata Nasibu (Diamond) anatoka tukawa tunazunguka naye kumsapoti, watu walisema tena ni bwanagu,” Queen Darleen aliambia EATV.


Mwisho

_________________________

_________________________



















================================================
Hatimaye Hapiness Magese afutwa machozi
Baada ya kufanyiwa operesheni zaidi ya 10 zilizotokana na tatizo la Endometriosis, Miss Tanzania 2001 na mwanamitindo wa kimataifa Happiness Magese amejifungua mtoto wa kiume akiwa kilogram 2 na gram 9, Alhamisi ya Julai 13 2117 huko nchini Marekani


Millen aliwahi kujitangaza hadharani kuwa ni muhanga wa tatizo la 'Endometriosis', tatizo ambalo huwakuta wanawake wengi pindi wanapoingia kwenye hedhi na kusababisha kuharikibika kwa mimba pia , na tatizo hili liliharibu mimba zake nyingi alizowahi kupata.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mrembo huyo aliandika,

"Mungu nakushukuru kwa kunifanya mwanamke na hatimaye nimekuwa mama, Mungu nakushukuru kwa kunirudishia baba yangu, jina lako lihimidiwe. Nampenda sana mwanangu, Prince Kairo Michael Magese amezaliwa saa 12 na dakika 58 asubuhi akiwa na uzto wa kilo 2 na gram 9, Julai 13, 2017,” sehemu ya ujumbe aliouandika Millen usiku wa kuamkia leo.


Happiness akiwa mjamzito.

Mrembo huyo amefanikiwa kupata mtoto huyo ikiwa na mtu ambaye alishakata tamaa na kuwahi kukiri mwaka jana kwenye chombo kimoja cha habari hapa nchini kwamba anataka kuondokana na maumivu ya kila mwezi kwa kuchagua njia ya kuondoa kizazi.

Tunampongeza sana Hapiness Magese kwa kumpata mtoto Kairo, ikiwa ni pamoja na kupambana katika kujitoa kwenye kutoa elimu juu ya ugonjwa wa Endometriosis.


Happiness Magese akiwa na mtoto wake mwenye umri wa wiki moja.


NA FATUMA MUNA


mwisho
=================================





About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search