Morning Talk: Mhe. Sugu kuibua Ajira Mpya' 5,000.. Mzee Lowasa amewasili Polisi hivi punde.. Kauli ya Mzee Mkapa 'yaliamsha Dude' haki za Binadam waja juu.. Jinamizi laikumba NSSF; Vigogo wake 11 watemwa... #share.. Kumbe Kidole cha Mguu kinaweza kuwa cha Mkono pia.. soma zaidi..

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop Bongo na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameweka wazi malengo yake kwa miaka 10 ijayo.



Sugu ambaye ni Mkurugenzi wa Hotel Desderia Co Ltd amebainisha hayo kupitia mtandao wa Instagram ambapo katika kipindi hicho amelenga kutoa ajira zisizopungua 5,000.

Rapper turned the Employer # This year I will employ about 50 of my fellow citizens… My goal is to employ not less than 5,000 in the coming 10 years, Inshallah… #DEIWAKA #JONGWE #MVMP
March mwaka jana Sugu aliweka wazi kuanza kwa ujenzi wa Hoteli yake yenye hadhi ya nyota tatu chini ya kampuni ya ukandarasi ya Home Africa Investment Co Ltd ya China - Bongo5
=============== end ========


Dar es Salaam. Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imewaachisha kazi wafanyakazi 12 waliokuwa wamesimamishwa kwa mwaka mmoja sasa.
Wafanyakazi hao walisimamishwa kazi Julai 2016 kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi.

Taarifa ya NSSF iliyotolewa leo Alhamisi (Julai 13) kupitia vyombo vya habari walioachishwa kazi ni Yacob Kidula, aliyekuwa mkurugenzi wa mipango, uwekezaji na miradi.

Wengine na nafasi walizokuwa wakishikilia kwenye mabano ni Ludocick Mrosso (mkurugenzi wa fedha), Chiku Matessa (mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala), Sadi Shemliwa (mkurugenzi wa udhibiti, hadhara na majanga), Pauline Mtunda (mkurugenzi wa ukaguzi wa hesabu za ndani).

Crescentius Magori (mkurugenzi wa uendeshaji), Amina Abdallah (meneja utawala), Abdallah Mselli (meneja wa uwekezaji), Mhandisi John Ndazi (meneja miradi), Wakili Chedrick Komba (meneja kiongozi Mkoa wa Temeke) na Ramadhani Nassibu (meneja mkuu usalama)




- Mwananchi Online
=============  end ===

Mfanyakazi mmoja wa shamba la ng'ombe ambaye kidole chake cha gumba kiling'olewa ana fahali, amefanyiwa upasuaji ambapo kidole chake ya mguu kilikatwa na kuhamishwa kwa kile cha mkono.


Zac Mitchell, 20, alijeruhiwa wakati akifanya kazi katika shamba moja lililo kijijini magharibi mwa Australia.
Alifanyiwa upasuaji mara mbili wa kurudisha kidole chake bila ya mafanikio kabla ya madaktari kuamua kuhamisha kidole chake cha mguu katika upasuaji uliodumu saa nane.
Bwana Mitchell alisema wafanyikazi wenake walijaribu kuhifadhi kidole mara baada ya ajali hiyo. Mitchel alisafirishwa kwa ndege hadi hospitali katika jimbo la Perth, lakini jitihada za kukiokoa kidole chake zikashindikana.Licha ya kukataa Mitchel baadaye alikubali kidole chake cha mguu kuhamishwa hadi kwa mkono wake.
Daktari wa upasuaji Sean Nicklin anasema hakushangazwa na muda aliochukua Mitchel kukukubali.
"Hata kama una vidole vinne vilivyo vyema, na huna kidole cha kifinyilia mkono wako utakuwa umepoteza sehemu kubwa ya kazi yake.
Bwana Mitchel atahitaji zaidi ya miezi 12 ya ushauri lakini na mpango wa kurudi shambani - BBC swahili

==============================


Mradi Mkubwa wa Umeme unaozalisha umeme mkubwa zaidi nchini China..
























About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search