Matukio Pichani: Ni sherehe na Vifijo Mama Salma akikabidhi Mikoba ya Tanzania Girls Guide kwa Mama Samia... #share
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wasichana ambo ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
Kauli hiyo aliitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa kijiti cha kuwa mlezi wa chama hicho kutoka kwa Mama Salma Kikwete anayesitaafu nafasi hiyo aliyoihudumu kwa zaidi ya miaka 12.
“Niwatake tu watoto wangu kutochukulia kwa mzaha mafunzo mnayopatiwa kwani ni tija kwa maendeleo ya Taifa,” alisema Makamu wa Rais.
Aidha aliwaahidi wanachama kutowaangusha katika kutekeleza majukumu ya kukilea chama hicho ambapo alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa kuweza kukiongoza vizuri kwa mafanikio makubwa licha ya kuwa na majukumu mengine - Na. Abraham Ntambala/Michuzi Blog.
Mama salma akimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mpango mkakati wa TGGA
Samia Suluhu Hasan akimkabidhi Mlezi mstaafu wa TGGA zawadi ya saa aliyopewa zawadi na uongozi wa TGGA kwa ajili ya kumbukumbu.
Kikundi cha sanaa cha Ilala kikitumbuiza
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye pia ni Kamishna wa TGGA, Sophia Mjema akimlaki aliyekuwa Mlezi wa TGGA Mama Salma Kikwete
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi
Salma Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna wa TGGA
Samia akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa na Girl Guides
Samia akipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi wa Girl Guides Ruth kuhusu kazi mbalimbali za TGGA
Viongozi mbalimbali wakiwa katika sherehe hiyo
Baadhi ya makamishna wa TGGA wakiwa katika sherehe hiyo
Mwenyekiti wa TGGA Profesa Martha Qorro akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Anna Abdalah akihutubia wakati wa sherehe hiyo
Aliyekuwa Mlezi wa TGGA, Mama Salma Kikwete akihutubia kabla ya kumkabidhi ulezi Makamu wa Rais Samia
Ni furaha iliyoje
Salma Kikwete akimvisha skavu Mlezi mpya wa TGGA, Samia Suluhu Hassan
Wasanii wa Shule ya Msingi Umoja wakitumbuiza wakati wa sherehe hiyo |
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema na Mwenyekiti wa Bodi ya TGGA, Anna Abdalah wakichenza ngoma |
Mama Samia akimtunza fedha kiongozi wa kikundi cha Umoja kwa kucheza vizuri
Kamishna Mkuu wa TGGA akimkabidhi zawadi ya saa Mlezi mstaafu wa TGGA, Mama Salma Kikwete
No comments:
Post a Comment