nEWS aLERT:: 72' Ya Lissu imetimia.. kikosi-kazi chini ya Lady-Lawyer Fatma Karume kujaribu kumnasua.. #share

Ni takriban masaa 72 kwa mara nyengine kikosi cha Mawakili takriban 18 chini ya 'mentor-ship' ya lady-lawyer Fatma Karume watakapojaribu tena kumnasua kwa dhamana Mwanansheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lissu, leo atakapopandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini hapa, kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili.


Lissu ambaye alikamatwa Ijumaa ya wiki iliyopita, anakabiliwa na kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa Jumatatu na kuahirishwa hadi leo huku wakili wake, Fatma Karume, akiwa na imani kuwa mteja wake atapewa dhamana.
Fatma amesema endapo Mahakama hiyo haitatoa dhamana kwa Lissu, watakata rufaa Makahama ya Rufaa.
Lissu anayetetewa na mawakili 18, anatuhumiwa kuwa Julai 17, akiwa mtaa wa Ufipa, Kinondoni alitoa lugha ya uchochezi hali ambayo ingesababisha chuki kwa sababu aligusa udini, ukabila na ukanda. 
Julai 24, Mbunge huyo alinyimwa dhamana na kutakiwa abaki rumande hadi leo ambapo Mahakama itatoa uamuzi wa dhamana, kutokana na upande wa Jamhuri kuwasilisha pingamizi. 
Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo, baada ya mawakili wa Lissu, Fatma na wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi na Saimon Wankyo kujibizana kwa hoja kwa zaidi ya saa mbili.
Baada ya majibizano hayo, Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi leo ili apitie hoja hizo na kuziandikia uamuzi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search