bREAKING nEWS: Yametimia.. 'Kamanda Lissu' wa (Chadema) aachiwa huru kwa dhamana ya Mil. 10 .. asitoke nje ya Jiji #share..

Mahakama ya Kisutu imemuachia huru kwa dhamana Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania Mh. Tundu Lissu.


Habari kutoka ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zitatonya Mbunge huyo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni ameachiwa kwa dhamana ya watu wawili wenye bondi ya Tshs. 10 Millioni kila mmoja.

Jopo la Mawakili zaidi ya 18 chini ya Lady_Lawyer Fatma Karume hapo awali siku ya tarehe 24/07/2017 waliambulia mikono mitupu licha ya kujipanga kihoja, jambo lililowalazimu kurejesha kikosi nyuma kwa masaa mengine 72.

=====================
MORE UPDATES:

Akitoa uamuzi huo hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri alisema upande wa mashtaka ulishindwa kutaja kesi ambayo Lissu aliwahi kuruka dhamana.

Kuhusu Lissu anyimwe dhamana kwa ajili ya  usalama wake, Hakimu Mashauri alisema sababu hiyo hajitoshelezi kumuweka ndani.

Alisema Lissu kundi la Mawakili 18 wamejitokeza kumuwakilisha na kwamba hiyo inaonesha  watu wanaupendo dhidi yake.

Hivyo amemtaka kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya sh 10 milioni kila mmoja.

Mshtakiwa asitoke nje ya jiji Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama.


Kesi imeahirishwa kwa muda kusubiri wadhamini ambao walifika lakini kutokana na ulinzi ulioimarishwa mahakani hapo na askari polisi walizuiwa kuingia...

Upande wa mashtaka umedai upelelezi umekamilika atasomewa maelezo ya awali (PH) Agosti 24,2017


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search